Pata taarifa kuu

DRC: Wanajeshi 6 waliohusika katika ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano wahukumiwa

Kesi ya wanajeshi sita wa FARDC nchini DRC, wakiwemo maafisa wawili wakuu, waliokamatwa baada ya kuhusika katika ukandamizaji dhidi ya maandamano uliyosababisha vifo vya watu 50 mnamo Agosti 30, ilianza kusikilizwa siku yaJumanne huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baadhi ya watu waliokamatwa wakati wa maandamano yaliyokandamizwa na vikosi vya ulinzi na usalama huko Goma, Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, Agosti 30, 2023.
Baadhi ya watu waliokamatwa wakati wa maandamano yaliyokandamizwa na vikosi vya ulinzi na usalama huko Goma, Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, Agosti 30, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ilianza mwanzoni mwa alasiri mbele ya mahakama ya kijeshi ya mkoa wa Kivu Kaskazini, katika chumba kilichojaa watu katika kambi ya kijeshi ya Katindo huko Goma, mji mkuu wa mkoa, ambapo tukio hilo lilitokea, amebainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Kesi yasitishwa jioni,na kuendelea Jumatano asubuhi

Washitakiwa hao ni maofisa wawili wa Jeshi la Jamhuri, Kanali Mike Mikombe na Luteni Kanali Donatien Bawili, ambao serikali ilitangaza kuwakamata kuwekwa chini ya ulinzi na askari wanne wa vyeo vya chini. Wote wanazuiliwa na walionekana mahakamani wakiwa wamevalia sare zao za kijeshi.

Alipoulizwa iwapo anatambua shutma zinazomkabili, Kanali Mikombe amejibu “hapana, sitambui”. Washtakiwa wengine bado hawajapewa nafasi ya kujibu au kujieleza.

Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani mara moja" baada ya kufunguliwa mashitaka hasa kwa "uhalifu dhidi ya binadamu", ametangaza hakimu mkuu katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Kanali Michel Kachil, anayewakilisha upande wa raia.

Amesema watu 56 waliuawa na 75 kujeruhiwa Jumatano ya wiki iliyopita wakati wa operesheni ya kijeshi iliyoanzishwa kuzuia maandamano yaliyopangwa na kanisa la Wazalendo dhidi ya uwepo wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Afrika Mashariki katika eneo hilo.

Operesheni hiyo ilifanywa kanisani na katika majengo ya redio ya dhehebu hili. Hati ya ndani ya jeshi iliripoti haraka watu 48 waliouawa na 75 kujeruhiwa, kabla ya serikali kutangaza idadi ya waliouawana 56 kujeruhiwa.

Walionusurika waliohojiwa Ijumaa iliyopita, walidai kuwa wanajeshi hao walifyatua risasi "bila maelezo" kwa makumi ya watu wasio na silaha.

Maafisa hao wawili wanaokabiliwa na mashitaka "walitoa mafunzo kwa askari wanne" kwa "vitendo hivyo viovu", amesema hakimu mkuu , na kuhakikisha kwamba "vitendo vyao vilitekelezwa kwa hiari yao wenyewe".

"Haikuwa hatua ya serikali, walifanya kwa hiari yao wenyewe," amesema.

Ujumbe wa mawaziri ulitumwa kutoka Kinshasa kwenda Goma Jumamosi "kutoa mwanga" juu ya matukio ya Agosti 30 na "kumhusisha kila mtu kwa makosa yake", kwa maneno ya serikali.

Mbali na kukamatwa kwa maafisa hao wawili wa kijeshi waliotangazwa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu huko Goma na Waziri wa Mambo ya Ndani Peter Kazadi, alitangaza Jumatatu jioni kuitishwa Kinshasa kwa "mashauriano" kwa gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Jenerali Constant Ndima, na kusimamishwa kazi kwa askari polisi wawili.

Kutoka New York, Farhan Haq, naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) "unahimiza kwa nguvu uchunguzi wa kina na huru" kuhusu suala hili na unafuatilia kesi hii inayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.