Pata taarifa kuu

Nchi wanachama wa Brics zinakutana nchini Afrika Kusini

Nairobi – Wanachama wa nchi zinazounda muungano wa mataifa ya Brics ikiwemo China, Urusi na India wanakutana nchini Afrika Kusini.

Jumla ya mataifa 69 yamealikwa katika mkutano huo yakiwemo yale ya Afrika.
Jumla ya mataifa 69 yamealikwa katika mkutano huo yakiwemo yale ya Afrika. via REUTERS - YANDISA MONAKALI/DIRCO
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unafanyika wakati huu nchi wanachama zikiwa zinawazia kuongeza idadi ya wanachama wake kama vile mataifa ya Iran na Argentina.

Wahusika kwa muungano huu wanaouna kama mbadala wa ubabe wa nchi za Magharibi katika taasisi za kidunia.

Tayari zaidi ya mataifa mapya 20 yameomba kujiunga na muungano huo mpya.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye anakabiliwa na kibali cha kukamatwa kutoka katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, hatahuduhuria kikao hicho binafsi kama ilivyotarajiwa.

Rais Lula wa Brazil pia anahudhuria
Rais Lula wa Brazil pia anahudhuria © flickr.com / BRICS

Viongozi kadhaa akiwemo rais wa China Xi Jiping, waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov wanahudhuria mkutano huo wa awamu ya 15.

Rais Xi alikaribishwa na mwenyeji wake rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Mapema siku ya Jumapili, rais Ramaphosa alisema Afrika Kusini haitalazimishwa kuegemea nchi zozote katika Nyanja ya kimataifa.

Jumla ya mataifa 69 yamealikwa katika mkutano huo yakiwemo yale ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.