Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Cyril Ramaphosa asifu faida ya BRICS kwa Afrika Kusini

Johannesburg inawapokea kuanzia Jumanne hii na hadi Alhamisi wakuu wa nchi za Brazil, China, India, na mkuu wa diplomasia ya Urusi, pamoja na viongozi wengine wa nchi za kusini, wakiwemo viongozi zaidi ya thelathini kutoka Afrika . Rais Cyril Ramaphosa alihutubia taifa katika hotuba ya televisheni siku ya Jumapili ili kufafanua mkakati wa serikali yake katika masuala ya uhusiano wa kimataifa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mnamo Julai 19, 2023.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mnamo Julai 19, 2023. via REUTERS - GCIS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Rais wa Afrika Kusini alirejelea katika moja ya masuala makuu yatakayokuwa kwenye ajenda ya mkutano huu wa 15 wa Brics, yaani suala la upanuzi wa kundi hilo, na uwezekano wa kutoa nafasi kwa nchi nyingine: "Zaidi ya nchi ishirini kutoka kote dunia wametuma maombi rasmi ya kujiunga na BRICS. Na Afrika Kusini inaunga mkono kuongeza wanachama. Toleo lililopanuliwa linaweza kuwakilisha kundi tofauti zaidi la mataifa, ambao wana mifumo tofauti ya kisiasa, na ambao wanachangia nia moja ya kuanzisha utaratibu wa ulimwengu uliosawazishwa zaidi. »

Zoezi la kusawazisha kwa upande wa Cyril Ramaphosa

Muungano wa Brics bado unatawaliwa na China, ambayo Cyril Ramaphosa anaifahamu vyema, kwa kuwa ziara ya rais Xi Jinping imepangwa Jumanne, wakati Beijing ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Pretoria: "Kuwa mwanachama wa BRICS kumeleta matumaini. fursa kwa nchi yetu ya Afrika Kusini. Na hilo limewezesha uchumi wetu kuunda ushirikiano wa kimkakati na China, nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani. "

Lakini pamoja na uhusiano huu, Cyril Ramaphosa hajasahau uhusiano wake muhimu wa kibiashara na nchi za Magharibi. Katika hatua ya kusawazisha, pia alitoa hoja ya kukumbusha, wakati wa hotuba hiyo, kwamba nchi yake itakuwa mwenyeji, mwezi wa Novemba, wa mkutano wa kilele wa AGOA kwa ushirikiano na Washington, pamoja na mkutano kati ya Afrika Kusini na Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.