Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu aomboleza vifo vya maafisa wa usalama 26

Nairobi – Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameomboleza vifo vya maafisa wa usalama 26, baada ya kuangushwa kwa helikopta ya kijeshi na watu wenye silaha katika jimbo la kati la Niger.

Rais Bola Tinubu amesema maofisa waliouawa walikuwa wamejitolea kwa ajili ya kulinda nchi.
Rais Bola Tinubu amesema maofisa waliouawa walikuwa wamejitolea kwa ajili ya kulinda nchi. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, wote waliouawa ni wanajeshi wa Nigeria na wanane walijeruhiwa. Maofisa hao walifariki wakati wakielekea katika shughuli za uokozi katika jimbo la Niger nchini Nigeria siku ya Jumatatu.

Rais Tinubu amesema wanajeshi hao waliouawa watakumbukwa kutokana juhudi zao za kuhakikisha raia wa taifa hilo wanaishi kwa amani.

Watalaam wa usalama wanazungumzia vipi tukio hili ?  George Musamali anathmini akiwa jijini Nairobi.

"Kuna changamoto mingi sana za kiusalama ndani na nje ya mipaka ya Nigeria na kwamab hivi sasa wamejitoa kifua mbele ya kwamba waingilia masula ya Niger kule ndani, shambulizi ambalo tunaliona, tunaweza kusema labda lina uhusiano nahali iliyoko kule nchini Niger." alisema George Musamali.

00:39

George Musamali kuhusu shambulio Nigeria

Helikopta hiyo iliyoanguka ilikuwa inaenda kuwaondoa wanajeshi wengine waliokuwa wameshambuliwa katika eneo moja ambapo jeshi limekuwa likipigana na makundi ya watu wenye silaha. Maofisa kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakiripotiwa kuwateka watu katikati na kaskazini mwa nchi ya Nigeria ambapo huitisha kikombozi ilikuwaachia huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.