Pata taarifa kuu

Wanajeshi nchini Nigeria wajeruhiwa kwenye shambulio la watu wenye silaha

Nairobi – Helikopta ya jeshi la Nigeria ambayo ilikuwa imetumwa kuwaokoa wanajeshi waliojeruhiwa kwenye shambulio mbaya katikati ya jimbo la Niger iliripotiwa kuanguka siku ya Jumatatu ya wiki hii baada ya kudaiwa kushambuliwa na watu wenye silaha.


Majambazi hao waliwavizia wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara ya kutoka Zungeru kuelekea Tegina katika jimbo la Niger.
Majambazi hao waliwavizia wanajeshi wa Nigeria kwenye barabara ya kutoka Zungeru kuelekea Tegina katika jimbo la Niger. © AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi kadhaa wameripotiwa kuawaua katika shambulio la kushtukiza katika eneo ambako jeshi limekuwa likikabiliana na makundi ya watu wenye silaha.

Vyanzo kutoka kwenye jeshi vimesema maofisa 26 wa usalama nchini Nigeria waliuawa wengine nane wakiripotiwa kujeruhiwa katika shambulio la siku ya Jumapili.

Vyombo vya habari vya ndani kwa upande wake vimerpoti kuwa karibia wanajeshi 13 waliuawa katika shambulio hilo la kuvizia.

Ndege hiyo ya uokozi ilikuwa imebeba miili 11 na maofisa wengine saba waliokuwa wamejeruhiwa kabla ya kuanguka.

Licha ya kutotoa taarifa kamili ya maofisa waliouawa, msemaji wa jeshi la angani nchini humo amesema oparesheni na uchunguzi zimeanzishwa kuhusiana na tukio hilo.

Makundi ya watu wenye silaha yamekuwa yakiripotiwa kuendeleza shughuli zake katikati na kaskazini Magharibi mwa Nigeria ambapo yanapora, kuwateka watu na baadae kuitisha kikombozi.

Maelfu ya watu wameripotiwa kuawaua katika mashambulio katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.