Pata taarifa kuu

Ethiopia: Hali ya wasiwasi yatanda kufuatia kuzuka kwa ghasia mpya Amhara

Nchini Ethiopia, takriban watu 26 waliuawa siku ya Jumapili Agosti 13 na shambulio la anga katika jimbo la Amhara. Jumatatu hii, Agosti 14, chombo cha ufuatiliaji wa haki za binadamu nchini Ethiopia - taasisi ya umma lakini huru kwa mujibu wa sheria zake - ndio ambayo ilionyesha 'wasiwasi wake mkubwa' kuhusiana na hali hii.

Moja ya maeneo katika jimbo la Amhara. Mei 2021.
Moja ya maeneo katika jimbo la Amhara. Mei 2021. © RFI/ Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Kuzuka upya kwa ghasia huko Amhara kati ya jeshi la shirikisho na wapiganaji wa ndani, lakini pia kukamatwa kwa watu wa kabila hili, kila mahali nchini,kumezua hali ya wasiwasi nchini kote Ethiopia.

Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia inabaini kwamba imepokea malalamiko kutoka kwa watu wa kabila la Amhara "kabla na baada ya kutangazwa kwa hali ya hatari", hali ya hatari iliyoamriwa mnamo Agosti 4, huko Amhara, na serikali ya shirikisho, katika hali ya mvutano unaoongezeka kati ya jeshi na vitengo vya wanamgambo.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed sasa anataka kuwasambaratisha wanamgambo hao, baada ya kuwategemea kwa miaka miwili wakati wa vita vya Tigray, eneo jirani la Amhara.

Tume hiyo pia inaripoti mapigano makali kwa siku kadhaa katika eneo la Amhara, huku kukiwa na mashambulizi makubwa ya mabomu na mashambulizi ya anga. Kulingana na shirika hilo, silaha nzito zilitumika, na kusababisha vifo na majeruhi wengi kati ya wakazi, pamoja na uharibifu.

Hakuna ripoti rasmi ya mapigano haya ambayo imetolewa.

Shirika la ufuatiliaji wa haki za binadamu la Ethiopia hatimaye limeripoti "kukamatwa kwa raia wengi wa asili ya Amhara" katika mji mkuu, Addis Ababa, na linasikitika kuwa halikupata  na nafasi ya " kubainisha mazingira yao ya kuzuiliwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.