Pata taarifa kuu

Nigeria: Watu saba wamefariki baada ya msikiti kuporomoka

Watu saba wamefariki baada ya  sehemu ya msikiti uliojaa mamia ya waumini ilipoporomoka katika mji wa kaskazini mwa Nigeria wa Zaria, katika jimbo la Kaduna, na wengine kadhaa kujeruhiwa, maafisa katika eneo hilo wamethibitisha.

Maafisa wa serikali walisema msikiti huo ulijengwa katika miaka ya 1830
Maafisa wa serikali walisema msikiti huo ulijengwa katika miaka ya 1830 AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea wakati mamia ya waumini walipokuwa wakisali sala ya alasiri siku ya Ijumaa katika msikiti wa kati wa jiji hilo.

Maafisa wa serikali walisema msikiti huo ulijengwa katika miaka ya 1830.

Kwa mujibu wa mamlaka katika eneo hilo, watu 23 tayari wamelazwa hosipitalini ambapo wanapokea matibabu.

Video zilizorekodiwa katika eneo la tukio zilionyesha mwanya mkubwa ambapo sehemu ya paa ilianguka.

Gavana wa jimbo la Kaduna Uba Sani aliagiza uchunguzi wa haraka kuhusu maafa hayo ufanyike na akaahidi kuwasaidia walioathirika na tukio hilo ambalo amelitaja kuwa kama la kuhuzunisha.

Tukio hilo linakuja baada ya majengo kumi kuporomoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika kipindi cha mwaka uliopita pekee.

Majanga kama haya hulaumiwa mara nyingi  kwa kushindwa kwa maofisa husika kutekeleza kanuni za usalama wa majengo na ujenzi duni na vifaa duni vya ujenzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.