Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Mgomo mkubwa wa teksi wazorotesha Cape Town na kusababisha vifo kadhaa

Mji wa Cape Town, ulioko kusini-magharibi mwa Afrika Kusini, umekwama kwa karibu wiki moja kufuatia mgomo wa madereva wa teksi. Kwa sababu SANTACO, shirika la madreva wa teksi nchini Afrika Kusini, limekasirika kwa sababu ya utumiaji wa kanuni na Halmashauri ya manispaa mji huo, unaoongozwa na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, kuruhusu magari yao kukamatwa endapo yatapaikana na kosa. Ghasia zimeongezeka tangu kuanza kwa mgomo huu na kusababisha vifo vya takriban watu watano.

Mgomo wa teksi ulizua vurugu kubwa mjini Cape Town, kama vile hapa, wakati wakazi wa Masiphumelele walipoweka vizuizi mnamo Agosti 8, 2023.
Mgomo wa teksi ulizua vurugu kubwa mjini Cape Town, kama vile hapa, wakati wakazi wa Masiphumelele walipoweka vizuizi mnamo Agosti 8, 2023. © Nic Bothma / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Takriban watu 120 wamekamatwa, huku takriban vifo vitano vimerekodiwa kando ya vuguvugu hili la mgomo, kulingana na polisi. Magari pia yalichomwa moto na maelfu ya wasafiri sasa wanajikuta wamekwama: teksi za pamoja ndio njia kuu ya usafiri kwa wakaazi wa Cape Flats, eneo kubwa linalojumuisha vitongoji vya jiji.

Shirika la SANTACO linataka kupinga kutumika kwa sheria ya Halmashauri ya manispaa ambayo inaruhusu mamlaka ya eneo hilo kukamata magari yanayokiuka - iwe kwa kuendesha gari bila leseni au kwa teksi ambayo haitimizi viwango. Mvutano uliongezeka wakati mabasi madogo 15 yalipokamatwa kwa siku moja wiki jana.

Serikali ya ANC, kupitia Waziri wake wa Uchukuzi, ilikubaliana na teksi za pamoja, ikizingatiwa kuwa kanuni hii mpya inakwenda zaidi ya uwezo wa manispaa. Hoja iliyokataliwa na jiji la Cape Town, ambayo inatoa wito kwa wawakilishi wa sekta hiyo kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Wito wa mgomo wa SANTACO bado unaendelea hadi siku ya Jumatano. Sherehe za Siku ya Wanawake wa Afrika Kusini, katika siku hiyo iliyo kuwa imepangwa awali mjini Cape Town, pia imehamishiwa Pretoria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.