Pata taarifa kuu

Shirika la ndege la Ethiopia limesitisha safari zake kwenye mji wa Amhara

Nairobi – Shirika la ndege la Ethiopia, limetangaza kusitisha safari zake kuelekea katika eneo la Bahir Dar, katika mji mkuu wa Amhara, likieleza kwamba halitatumia viwanja vyovyote vya ndege katika eneo hilo kutokana na machafuko kati ya makundi ya watu wenye silaha na wanajeshi wa serikali.

Machafuko mapya yamekuwa yakiripotiwa katika mji wa Amhara kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali
Machafuko mapya yamekuwa yakiripotiwa katika mji wa Amhara kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali AFP PHOTO/JENNY VAUGHAN.
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya wiki jana, shirika hilo la ndege la kitaifa kusitisha safari zake katika viwanja vingine vitatu vya ndege kaskazini mwa taifa hilo.

Serikali ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wiki iliyopita ilitangaza kipindi cha miezi sita cha hali ya dharura katika eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa machafuko.

Machafuko haya mapya nchini humo yanakuja ikiwa imepita miezi tisa tangu kumalizika kwa mapigano mengine yaliodumu kwa kipindi cha miaka miwili katika jimbo jirani la Tigray.

Wasiwasi imekuwa ikiongezeka tangu mwezi Aprili baada ya serikali ya shirikisho kutangaza kuvunjwa kwa vikosi vya majimbo nchini humo.

Hatua hiyo ya serikali ilisababisha maandamano katika eneo la Amhara, raia wake wakisema hatua hiyo ingedhoofisha eneo lao.

Baadhi ya serikali za kigeni zimewataka raia wake kuwa makini na kuchukua tahadhari wanaposafiri kuelekea kwenye eneo hilo.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.