Pata taarifa kuu

Mapinduzi Niger: ECOWAS yaitisha mkutano mpya, Mali na Burkina Faso kutuma wajumbe Niamey

Saa chache baada ya kumalizika kwa makataa yaliyotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger, ECOWAS imeitisha mkutano wa pili wa wakuu wa nchi kuhusu hali nchini Niger hadi Agosti 10. Mnamo Agosti 7, 2023, vikosi vya wanajeshi wa Mali (Fama) pia vilitangaza kwamba Burkina Faso na Mali zitatuma ujumbe huko Niamey, "kuonyesha mshikamano wa nchi hizo mbili kwa raia wa Niger".

Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wakiwa katika kikao kisicho cha kawaida mjini Abuja, Julai 30, 2023.
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wakiwa katika kikao kisicho cha kawaida mjini Abuja, Julai 30, 2023. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS imeitisha mkutano mpya wa Wakuu wa Nchi na Serikali, Alhamisi ijayo, Agosti 10 huko Abuja, kuhusu hali nchini Niger.

Mkutano huo unatakuja siku chache baada ya kumalizika kwa makataa yaliyotolewa na ECOWAS kwa viongozi wa mapinduzi ili kurejesha mamlaka na kumrejesha tena mamlakani Mohamed Bazoum, aliyepinduliwa Julai 26.

Huu utakuwa ni mkutano wa pili wa wakuu wa nchi kuitishwa chini ya wiki mbili, baada ya ule wa Julai 30. Kulingana na vyanzo vya RFI, nchi wanachama zimearifiwa na ujumbe kutoka kwa tume ya ECOWAS.

Ni mkutano uliopangwa mjini Abuja, katika nchi ya Bola Tinubu, rais wa Nigeria, mwenyekiti wa ECOWAS.

Mambo hayaendi jinsi jumuiya hiyo linavyotaka, huku majaribio ya upatanishi yakishindwa. Duru za kuaminika zinabaini kwamba, viongozi wa mapinduzi wanawasilisha kurejea kwa Rais Mohamed Bazoum kama kikwazo.

Mnamo Agosti 5, Bunge la Seneti la Nigeria pia lilisema haliungi mkono uingiliaji kati huo wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.