Pata taarifa kuu

HRW yawathumu walinda usalama nchini Angola kwa mauaji ya wanaharakati

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limewatuhumu maofisa wa polisi nchini Angola kwa kutekeleza mauaji ya watetezi wa haki za watu tangu mwezi Januari na kutoa wito kwa serikali kuchunguza ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu.

HRW imesema walinda usalama nchini humo pia wametuhumiwa kwa kuwakamata na kuwazuia  mamia ya watetezi za haki za watu
HRW imesema walinda usalama nchini humo pia wametuhumiwa kwa kuwakamata na kuwazuia  mamia ya watetezi za haki za watu © HRW
Matangazo ya kibiashara

Aidha HRW imesema walinda usalama nchini humo pia wametuhumiwa kwa kuwakamata na kuwazuia  mamia ya watetezi za haki za watu.

Polisi, maofisa wa ujajusi na wale wa kutoka vitengo vingine vya usalama wanadaiwa kutekeleza mauaji ya karibia watu 15 kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo.

Watu waliolengwa pakubwa na vyombo vya usalama  nchini humo ni pamoja na wanaharakati wa kisiasa, na wale waliotuhumiwa kwa kupanga maandamano, suala ambalo HRW imelaani.

Licha ya serikali ya Angola  kujaribu kuboresha masuala ya kisheria, haijakuwa rahisi kuwajibisha maofisa wa polisi wanaotuhumiwa kwa kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu.

Ripoti za watu kukamatwa zimeripotiwa pakubwa katika eneo lenye utajiri wa mafuta katika jimbo la Cabinda kaskazini mwa taifa hilo , mpaka na DR Congo.

Katika kipindi cha wiki sita zilizopita, shirika hilo limewahoji watu 32 nchini humo wakiwemo waathiriwa na familia zao, walioshuhudiwa pamoja na vyanzo vya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.