Pata taarifa kuu

Viongozi wa Afrika watoa wito wa kufufuliwa kwa mkataba wa Bahari nyeusi

Nairobi – Viongozi wa Afrika wanaohusika katika juhudi za upatanishi wa mzozo wa Ukraine, wametoa wito wa kutolewa suluhu ngano na mbolea kutoka Urusi ili kufufua mkataba wa kimataifa wa eneo la Bahari nyeusi, nchi ya Afrika Kusini imesema.

Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kupatikana kwa muafaka kuhusu mzozo wa Ukraine
Viongozi wa Afrika wamekuwa wakitaka kupatikana kwa muafaka kuhusu mzozo wa Ukraine via REUTERS - HOST PHOTO AGENCY RIA NOVOSTI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao, viongozi 6 walioenda Moscow na Kiev, pia wanautaka umoja wa Mataifa, kuagiza kuachiliwa kwa tani laki 2 za mbolea ya Urusi zinazoshikiliwa katika bandari za Ulaya.

Aidha, msemaji wa rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, amesema viongozi hao wanataka kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya nafaka na mbolea kutoka Urusi, vikwazo ambavyo vikiondolewa Moscow huenda ikarejea kutekeleza makubaliano ya awali.

Mwezi uliopita Urusi ilijitoa katika mkataba huo uliokuwa chini ya Umoja wa Mataifa nan chi ya Uturuki, Moscow ikitaka kwanza kupewa hakikisha la kuuza na kusafirisha mbolea na nafaka zake katika soko la dunia.

Haya yanajiri wakati huu Jumuiya ya kimataifa ikionya kuhusu uwezekano wa nchi masikini kukumbwa na njaa hasa za bara la Afrika ambalo linategemea kwa sehemu kubwa nafaka kutoka kwenye mataifa hayo mawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.