Pata taarifa kuu

ECOWAS yaapanga kuingilia kati kijeshi nchini Niger

Uingiliaji kati wa kijeshi nchini Niger ni "chaguo la mwisho ambalo liko mezani" kumrejesha mamlakani rais Mohamed Bazoum, aliyepinduliwa kupitia mapinduzi ya kijeshi wiki moja iliyopita, amesema afisa kutoka ECOWAS, Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ambayo viongozi wake wametishia kutumia "nguvu". Wakati huo huo, misaada ya kimataifa inaendelea kusitishwa, huku Benki ya Dunia ikitangaza kusitisha kutoa msaada wowote kwa Niger.

Rais wa Nigeria na ambaye pia ni rais wa ECOWAS Bola Tinubu, wakati wa kikao kisicho kuwa cha kawaida mjini Abuja, Julai 30, 2023.
Rais wa Nigeria na ambaye pia ni rais wa ECOWAS Bola Tinubu, wakati wa kikao kisicho kuwa cha kawaida mjini Abuja, Julai 30, 2023. © AFP/Kola Sulaimon
Matangazo ya kibiashara

"Chaguo la kijeshi ni chaguo la mwisho kabisa ambalo linajadiliwa, suluhu la mwisho, lakini lazima tujitayarishe kwa tukio hili," anasema Kamishna wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa na Usalama, Abdel. -Fatau Musah. Alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa majeshi kutoka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, mjini Abuja, Nigeria, unaotarajiwa kumalizika iku ya Ijumaa, siku mbili kabla ya kumalizika siku ya Jumapili kwa makataa ya ECOWAS ya kutaka kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba. 

Huko Niamey, mkuu wa wanajeshi waliochukua madaraka, Jenerali Abdourahamane Tchiani, alitangaza " kutupilia mbali vikwazo" na "kukataa kuachia ngazi kwa tishio lolote", katika hotuba ya televisheni, kwenye mkesha wa maadhimisho ya uhuru wa nchi hiyo, koloni la zamani la Ufaransa, leo Alhamisi. "Tunakataa kuingiliwa kwa aina yoyote katika masuala ya ndani ya Niger, " amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.