Pata taarifa kuu

Nigeria: Maandamano ya kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta yafanyika

Nchini Nigeria, wanachama wa vyama vya wafanyakazi wanaandamana kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na mfumuko wa bei unaosababishwa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.:

Bei ya mafuta imeonekana kupanda nchini Nigeria baada ya serikali ya rais Tinubu kuondoa ruzuku kwa bidhaa hiyo
Bei ya mafuta imeonekana kupanda nchini Nigeria baada ya serikali ya rais Tinubu kuondoa ruzuku kwa bidhaa hiyo AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya mazungumzo kati ya miungano hiyo na serikali kukosa kuafikia suluhu siku ya Jumanne.

Kiongozi wa muungano wa wafanyikazi nchini Nigeria Joe Ajaero aliwataka wanachama wake "kukusanyika katika majimbo yote nchini kote kutoa azimio hilo la pamoja".

Mkuu wa polisi Kayode Egbetokun alionya dhidi ya ghasia wakati wa maandamano hayo na kuwataka maofisa wake kuwalinda waandamanaji.

Vyama vya wafanyakazi vimesema hatua  zilizotangazwa na Rais Bola Tinubu siku ya Jumatatu ili kupunguza athari za kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta hazikutosha.

Serikali ilisema kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kutasaidia kupunguza mzozo wa ufadhili wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.