Pata taarifa kuu

Serikali ya DRC yaridhishwa na maandalizi ya michezo ya Francophonie

Nairobi – Michezo ya Francophonie imeanza rasmi jijini Kinshasa, nchini DRC huku waziri wa mambo ya nje Christophe Lutundula akifurahishwa na njinsi ambavyo serikali imefanikisha michezo hiyo licha ya changamoto za kifedha na hali ngumu ya uchumi.

Michezo hii inafanyika baada ya kuahirishwa mwaka 2021 kutokana na janga la Uviko 19
Michezo hii inafanyika baada ya kuahirishwa mwaka 2021 kutokana na janga la Uviko 19 © RFI/Ndiassé SAMBE
Matangazo ya kibiashara

Msikilizaji mamia ya raia wa DRC, walijitokeza hivi leo katika sherehe za ufunguzi wa michezo ya la Francophgonie inayofanyika jijini Kinshasa, michuano inayong’oa nanga licha ya wasiwasi wa usalama.

Baadhi ya mataifa yalioaalikiwa yalisusia michezo hiyo kwa hofu ya usalama
Baadhi ya mataifa yalioaalikiwa yalisusia michezo hiyo kwa hofu ya usalama © Ikulu ya kinshasa

Michezo hii ambayo inahusisha wanamichezo kutoka mataifa hasa yanayozungumza Kifaransa, inafanyika kwa mara ya kwanza kwenye taifa hilo la Afrika ya kati.

Rais wa DRC na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa michezo
Rais wa DRC na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria ufunguzi wa michezo © Patrick Muyaya

Christophe Lutundula, waziri wa mambo ya nje wa DRC alikuwa na kauli hii wakati wa hafla ya ufunguzi ya michezo hiyo.

‘‘Baada ya Ivory Coast, shirika la Francophonie lilijipata katika wasiwasi kwa kushindwa kuandaa michezo hii ya tisa lakini mkuu wa nchi aliamua kutoa ukarimu wa watu wa Kongo ilikufanyika kwa michezo hii, ni mkutano muhimu sana kwa wanaozungumza lugha ya kifaransa.’’ alisema Christophe Lutundula.

00:36

Christophe Lutundula, waziri wa mambo ya nje wa DRC

Usalama uliimarishwa nje ya uwanja ambako sherehe zimefanyika, ambapo watu wanakadiriwa kufikia elfu 80 wanatarajhiwa kufuatilia michezo hiyo.

Kwa juma zima, msemaji wa serikali na waziri wa mawasiliano Patrick Muyaya, alisisitiza nchi yake kuwa tayari kuhodhi mashindano hayo, akisisitiza uwepo wa usalama wakati wote wa michezo hiyo.

Michezo hiyo inafanyika wakati huu baada ya kuhairishwa awali kutokana na janga la uviko 19
Michezo hiyo inafanyika wakati huu baada ya kuhairishwa awali kutokana na janga la uviko 19 © Patrick Muyaya

Michezo hii inafanyika baada ya kuahirishwa mwaka 2021 kutokana na janga la Uviko 19, huku pia ikigubikwa na siasa kati ya Rwanda na DRC, ambapo katibu mkuu wa shirika la La Francophonie, raia wa Rwanda Louis Mushikiwabo, hatahudhuria

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.