Pata taarifa kuu

Niger: Katibu mkuu wa UN aelezea wasiwasi kuhusu mapinduzi ya kijeshi

Nairobi – Hatua ya jeshi nchini Niger, kutangaza kumwondoa madarakani rais Mohamed Bazoum, imeendelea kulaaniwa, huku mataifa mbalimbali yakiongozwa na Ufaransa na Marekani, yakiendelea kushinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi huyo na kurejeshwa na utawala wa kawaida wa kiraia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress anasema kinachotokea Niger, kinatishia usalama wa ukanda wa Sahel.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress anasema kinachotokea Niger, kinatishia usalama wa ukanda wa Sahel. REUTERS - BRENDAN MCDERMID
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa haijafahamika vema ni nani anayeongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi, baada ya rais Bazoum kuapa jana kuendelea kuilinda demokrasia ya nchi hiyo. 

Hata hivyo, uongozi mkuu wa jeshi umetangaza kuunga mkono hatua ya kundi la wanajeshi waliotangaza kumpindua rais Bazoum. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress anasema kinachotokea Niger, kinatishia usalama wa ukanda wa Sahel. 

“Kwa kweli nina wasiwasi ukiangalia Ukanda huo unapataka kwamba kuna magaidi ambao wanaendelea kufanya maovu kule Mali, Burkina Faso, Niger na sasa wanakaribia mataifa ya pwani, hali isioeleweka ya mpito kule Chad na hali ya kutisha nchini Sudan.” amesema katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

00:33

Antonio Guteress, Katibu mkuu wa UN

Mkuu huyo wa UN amesema eneo lote la jangwa la Sahara linaendelea kuwa tete, raia wakiripotiwa kuathiriki na kutatiza amani katika bara la Afrika.

 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya ECOWAS, pia zinashikiza kuachiwa kwa rais Bozoum na kurejeshwa kwa hali ya kawaida nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.