Pata taarifa kuu

Nigeria: Madaktari katika sekta ya umma wameanza mgomo

Wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika hosipitali za umma nchini Nigeria, wameanza mgomo kulalamikia kile wanachosema ni hatua ya serikali kushindwa kushugulikia matakwa yao.

Madkatari hao wanasema serikali imekosa kushugulikia matakwa yao
Madkatari hao wanasema serikali imekosa kushugulikia matakwa yao © AFP
Matangazo ya kibiashara

Asilimia kubwa ya madktari katika taifa hilo la Afrika Magharibi wameajiriwa na serikali na mgomo huu inahofiwa kuwa huenda ukalemeza shughuli katika sekta hiyo muhimu.

Sehemu kubwa ya raia katika nchi za Afrika wanategemea huduma za matibabu kutoka katika hosipitali za umma, wengi wakisema wanafanya hivyo kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha, hatua ambayo haiwaruhusu kutafuta huduma katika  hosipitali za kibnafsi.

Maofisa hao wanataka kulipwa mara moja kwa mishaara yao pamoja na kupewa marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu.

Kwa mujibu wa muungano wa madaktari nchini Nigeria, karibia wanachama wake 50 huondoka nchini humo kila wiki kwenda kutafuta mazingira bora ya kufanya kazi katika nchi za kigeni.

Mazingira mabovu ya kazi pamoja na malipo duni na kupanda kwa gharama ya maisha ni baadhi ya sababu zinazopelekea wahudumu wa afya kuondoka nchini Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.