Pata taarifa kuu
USALAMA-MAZINGIRA

DRC: Mashirika yaonya kuhusu visa vya uporaji katika Hifadhi ya Virunga

Nchini DRC, mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na mazingira yameitahadharisha serikali kuhusu visa vya uporaji vinavyoripotiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Virunga na makundi yenye silaha na hasa waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, kulingana na ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa.

Mlima Nyiragongo na Safu za Virunga katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga karibu na Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mlima Nyiragongo na Safu za Virunga katika Mbuga ya Kitaifa ya Virunga karibu na Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Getty Images - Chris Dennis Rosenberg
Matangazo ya kibiashara

Katika barua iliyotumwa kwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Félix Tshisekedi, wiki iliyopita, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na mazingira yanashutumu harakati za watu wenye silaha, pamoja na mambo mengine, ujangili, usafirishaji wa kuni na mkaa na hata usafirishaji wa nyani watoto, katika sehemu hii inayolindwa kinadharia iliyoko mashariki mwa nchi.

Hiki ni kilio cha kweli kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikalinchini DRC. Wana wasiwasi kuhusu mustakabali wa Hifadhi ya Virunga. Kwa mujibu wa Corneille Semakuba, mratibu katika Kituo cha Utafiti wa Mazingira, Demokrasia na Haki za Kibinadamu (CREDDHO), lazima tukomeshe uharibifu ambao umefanyika tangu kuanza kwa vita dhidi ya M23.

“Pamoja na kuwasili kwa kundi la waasi la M23, matukio ya ujangili yameongezeka, kuna ukataji miti na uharibifu mkubwa. Kumekuwa na biashara haramu ya nyani watoto. Na kuna baadhi ya wanyama ambao wameacha mazingira yao ya asili na kukimbilia nchi jirani, kama vile Rwanda. Nyani wengi wamevuka mpaka kufuatia kuwepo kwa makundi yenye silaha na M23 katika sehemu hii,” anaelezea Corneille Semakuba.

'Uhalifu wa mazingira lazima pia uzingatiwe'

Kama M23 itanyooshewa kidole kwa uhalifu huu, Corneille Semakuba pia anataja makundi mengine yenye silaha au vikosi vya jeshi vinavyohatarisha uwiano wa Virunga. Na mwanaharakati huyo wa mazingira anatoa onyo, kabla ya kukaribia kuwasili kwa wanajeshi wapya wa kigeni katika eneo hilo.

“Tunatoa tahadhari hii ili rais wa Jamhuri azingatie kile kinachoharibiwa huko, na uporaji unaofanywa ili askari wapya watakaokuja watambue hili na wasiingie kwenye uharibifu wa Hifadhi ya taifa. Kwa sababu ikiwa tutaongeza wanajeshi zaidi kujiunga na wanajeshi waliopo katika eneo hilo, likiwemo pia kundi la M23, mbuga yetu, urithi wetu wa ulimwengu, utaendelea kuwa hatarini, "anaongeza Corneille Semakuba.

Creddho inaomba mamlaka ya Kongo kuwa macho kuhusu utaratibu wa kisheria. "Uhalifu wa kimazingira lazima pia uzingatiwe wanapowahukumu waliohusika na ghasia," amebaini Corneille Semakuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.