Pata taarifa kuu

Serikali ya Nigeria kuwakinga raia wake kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta

Nairobi – Serikali ya Nigeria inasema itaanza kusambaza nafaka na mbolea wiki ijayo ikiwa ni njia moja ya juhudi zake za kuwakinga raia wa taifa hilo kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, hali iliyosababishwa na hatua ya rais Tinubu kuondoa ruzuku ya petrol.

Nigeria imekuwa inakabiliwa na kupanda kwa bei ya mafuta tangu serikali kuondoa ruzuku ya bidhaa hiyo
Nigeria imekuwa inakabiliwa na kupanda kwa bei ya mafuta tangu serikali kuondoa ruzuku ya bidhaa hiyo AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Bei ya bidhaa za kimsingi zimeonekana kupanda, sekta ya uchukuzi na huduma zengine zikiripotiwa kuathirika.

Aidha serikali  inasema inawazia mapendekezo ya kuwaongezea mishaara wafanyikazi wa serikali.

Raia nchini Nigeria wanaonekana kuaanza kukerwa na hatua ya kupanda kwa gharama ya maisha, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hatua hii ya Serikali mpya ya rais Bola Tinubu inalenga kuonyesha kwamba inalishugulikia tatizo hilo.

Serikali ya rais Bola Tinubu, inasema inashugulikia suala la kupanda kwa bei ya mafuta
Serikali ya rais Bola Tinubu, inasema inashugulikia suala la kupanda kwa bei ya mafuta REUTERS - TEMILADE ADELAJA

Pamoja na mipango mengine, serikali ya Tinubu inapanga kuzipa pesa familia masikini ila kwanza anataka ukaguzi kufanyiwa sajili ya watu wanaopendekezwa kufaidika na mpango huo.

Serikali pia inapanga kuanzisha usafiri wa mabasi yanyotumia umeme kama njia moja ya kupunguza gharama ya usafiri.

Vyama vya wafanyikazi vimekashifu hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta bila ya kuwepo kwa mpango muafaka wa kukabiliana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.