Pata taarifa kuu

DRC: Mashindano ya Francophone kuaanza tarehe 28 Julai

Nairobi – Ikiwa imesalia wiki moja kabala ya kuaanza kwa michezo ya Francophone, wafanyikazi jijini Kinshasa wameonekana kuwa mbioni kukamilisha baadhi ya sehemu ambazo ni muhimu kuelekea mashindano hayo ambayo ni sawa na yale ya Jumuiya ya madola.

DRC itakuwa mwenyeji wa michezo ya Francophonie mwaka huu
DRC itakuwa mwenyeji wa michezo ya Francophonie mwaka huu REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Karibia wanariadha elfu tatu kutoka katika mataifa 30 wanatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuelekea ufunguzi wa mashindano hayo tarehe 28 ya mwezi Julai.

Wafanyikazi wa kupaka rangi, mafundi wa mitambo na wahudumu wengine wameonekana wakiwa mbioni kumalizia sehemu zilizosalia, washiriki wengine wakiwa wamejiondoa kwa hofu ya usalama wao.

Mazoezi ya sherehe za ufunguzi hata hivyo yameanza katika uwanja wa Stade des Martyrs, ambao AFP iliutembelea wakati wa ziara iliyoongozwa na wanahabari na mabalozi wa kigeni siku ya Alhamisi.

Hofu ya awali kwamba hafla hiyo ya siku 10 itasitishwa inaonekana kupungua.

DRC ilichaguliwa mnamo 2019 kuwa mwenyeji wa mashindano ya awamu ya  tisa ya Francophone, hafla inayofanyika kila baada ya miaka minne ambayo inajumuisha  michezo na utamaduni.

Wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu nchini DRC
Wanariadha elfu tatu wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu nchini DRC (Photo: Reuters)

Hapo awali michezo hiyo ilipangwa kufanyika mnamo 2021, lakini iliahirishwa kwa sababu ya janga uviko 19 na ikacheleweshwa tena mwaka jana kwa sababu vifaa havikuwa tayari.

Waziri wa mambo ya nje wa Kongo Christophe Lutundula aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi kwamba kukusanya pamoja fedha ili kuandaa hafla ya kimataifa ya michezo ni vigumu "unapokuwa nchi kwenye vita".

Makundi yenye silaha yameonekana kuwa changamoto kwa usalama mashariki ya taifa hilo, vikosi vya Afrika Mashairiki vikiwa vimetumwa nchini humo kuwakabili waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.