Pata taarifa kuu

Ghana imetetea uamuzi wa kuwafukuza waomba hifadhi wa Burkina Faso

Ghana imetetea mpango wake wa kuwarejesha waomba hifadhi wanaotokea nchini Burkina Faso,baada ya shirika umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi kuitaka serikali kusitisha hatua hiyo.

Serikali ya Ghana inasema inawaondoa waomba hifadhi walioingia nchini mwake kinyume na sheria
Serikali ya Ghana inasema inawaondoa waomba hifadhi walioingia nchini mwake kinyume na sheria AP - Jacquelyn Martin
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa usalama wa kitaifa nchini Ghana katika taarifa yake amesema washukiwa wa ugaidi na wahamiaji haramu walikuwa wanarejeshwa kwao kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.

Aidha mamlaka nchini humo imesema wakimbizi wanaotaka kurejea kwao ndiyo wanaruhusiwa.

Burkina Faso inakabiliwa na utovu wa usalama unaotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha ambao Ghana inahofia kuwa wanaweza chukua fursa hiyo kupenyeza nchini humo kama wakimbizi.

Zaidi ya milioni mbili wamekimbia makwao nchini Burkina Faso  kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama. Baadhi, hasa wanawake na watoto, wametafuta hifadhi kaskazini mwa Ghana.

Burkina Faso ni mojawapo ya nchi kadhaa za Afrika Magharibi zinazopigana na makundi yenye silaha yaliyokita mizizi kaskazini mwa Mali katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, na kuua maelfu ya watu wakati wengine  zaidi ya milioni sita wakiwa wametoroka makazi yao.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Aliliambia gazeti hilo hakuna uwezekano wa Wagner kubaki katika hali yake ya sasa.

"Wagner hayupo," Putin alimwambia Kommersant. "Hakuna sheria juu ya mashirika ya kijeshi ya kibinafsi. Haipo tu.”

Prigozhin haijulikani kwa sasa na, hadi wiki iliyopita, vikosi vyake vilikuwa bado vijachukua ofa ya kuhamia Belarusi.

Siku ya Jumatano, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema Wagner alikuwa akikamilisha kukabidhi silaha nzito kwa wanajeshi wa kawaida wa Urusi huku Pentagon ikisema kuwa jeshi la mamluki halishiriki katika operesheni za kijeshi nchini Ukraine kwa njia yoyote muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.