Pata taarifa kuu

UNHCR yatoa wito kwa Ghana kutowafukuza wakimbizi wanaotoka Burkina Faso

Nairobi – Shirika la kutetea haki za wakimbizi katika umoja wa mataifa (UNHCR) limetoa wito kwa mamlaka nchini Ghana kutowafukuza nchini humo wakimbizi wanaotoroka utovu wa usalama nchini Burkina Faso.

Burkina Faso imekuwa ikakbiliwa na changamoto la kiusalama kwa muda sasa
Burkina Faso imekuwa ikakbiliwa na changamoto la kiusalama kwa muda sasa © RFI
Matangazo ya kibiashara

UNHCR katika taarifa yake imeelezea kuguswa na ripoti kwamba mamia ya raia wa Burkina Faso wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wamefukuzwa nchini Ghana ambako walikuwa wameenda kutafuta usalama.

UN imesema iko tayari kuisaidia nchini ya Ghana kukabiliana na changamoto la wakimbizi.

Zaidi watu milioni mbili nchini Burkina Faso wametoroka makazi yao kwa kuhofia mashambulio yanayotekelezwa na makundi ya kijahadi.

Ukanda wa Sahel umekuwa ukitatizwa na changamoto la kiusalama kutoka kwa makundi ya watu wenye silaha wanaoshambuliwa makazi ya raia na kutekeleza mauaji.

Burkina Faso na mataifa mengine kama vile Mali na Niger yamekuwa yakitatizwa na makundi ya kijihadi yanaoendeleza shughuli zao hadi katika mataifa jirani ikiwemo Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.