Pata taarifa kuu

Hali ya usalama Darfur imekwamisha juhudi za kusambaza misaada :WFP

Nairobi – Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa hali ya usalama katika eneo la Darfur nchini Sudan, imekwamisha juhudi za kusambaza misaada kwa waathiriwa wa mapigano yanayoendelea nchini humo.

WFP inasema zoezi la usambazaji wa chakula cha msaada katika jimbo la Darfur linatatizwa na utovu wa usalama
WFP inasema zoezi la usambazaji wa chakula cha msaada katika jimbo la Darfur linatatizwa na utovu wa usalama AFP PHOTO / CHARLES LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na WFP, wamefanikiwa kusambaza misaada kwa zaidi ya watu laki 4 katika maeneo ya mashariki, kaskazini, kusini na katikati mwa Darfur.

Idadi kubwa ya raia wanaowasili nchini Chad kutoka Darfur wamejeruhiwa vibaya huku kukiwa na ripoti kwamba raia wanaokimbia wanalengwa kimakusudi wakati huu ongezeko la kikabila vurugu likiripotiwa.

WFP imekuwa ikifanya kazi na washika dau katika sekta ya  afya na serikali ya mitaa kuboresha miundombinu ya afya katika mpaka wa Chad na Sudan.

Hadi sasa WFP imejenga mahema sita ya muda, yakiwemo mawili yanayotumika kama hospitali ya muda na vifaa vya matibabu, na manne kama sehemu za kupita kwa wakimbizi wapya wanaovuka kuingia Chad.

Stephan Dujaric ni msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

‘‘Wakati mapigano yakiendelea, maelfu ya watu wameendelea kuingia nchini Chad wakitokea eneo la Darfur, WFP imezidisha usambazaji wa misaada ilikuwasaidia watu wanaoingia katika maeneo ya mipaka.’’ alisema Stephan Dujaric ni msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.

00:29

Stephan Dujaric ni msemaji wa katibu mkuu wa UN

Kuna viwango vya juu vya utapiamlo miongoni mwa watoto wanaovuka kutoka Darfur kwenda Chad. Takwimu zinaonyesha zaidi ya asilimia 10 ya watoto wana utapiamlo.

Msimu wa mvua umeanza kuleta changamoto kwa shughuli za usafiri katika barabara kwenye mpaka wa Chad-Sudan.

WFP inatoa msaada wa chakula na lishe kwenye eneo la Darfur Mashariki, Kaskazini, Kusini na Kati, huku zaidi ya watu 420,000 wakiwa wamesaidiwa  hadi sasa, ila kwa sasa suala la usalama limekuwa tatizo kwa WFP Darfur Magharibi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.