Pata taarifa kuu

Ethiopia: Jimbo la Tigray linakabiliwa na hali ya njaa baada ya vita vya muda mrefu

Nairobi – Eneo la Tigray nchini Ethiopia, limeendelea kukumbwa na hali ya njaa baada ya vita vya muda mrefu, kutokana na kusitishwa kwa shughuli za usambazaji wa misaada ya kibinadamu, hali ambayo imesababisha kudhoofika kwa hali ya kiafya ya raia katika eneo hilo.

Mashirika ya misaada yalitangaza kusitisha usambazaji wa chakula nchini humo kwa madai kuwa kinaporwa
Mashirika ya misaada yalitangaza kusitisha usambazaji wa chakula nchini humo kwa madai kuwa kinaporwa AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Usambazaji wa misaada ya kibinadamu ilirejelewa Novemba mwaka jana baada ya kuafikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Hata hivyo kulingana na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, shughuli hiyo ilisitishwa tena mapema mwaka huu kutokana na madai kuwa misaada hiyo haikuwa ikiwafikia walengwa kutokana nabaadhiya watu kujilimbikizia misaada hiyo na kuyauza kwenye masoko nchini humo.

Kulingana na daktari, Gebrehiwot Gebregziaher, anayesimamaia tume ya tume ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari ya majanga katika eneo la Tigray, kuanzia mwezi Aprili na Mei, tume hiypo ilikuwa imepokea ripoti ya kufariki watu 595 kutokana na njaa kutoka wilaya kadhaa eneo hilo.

Kulingana na WFP, takriban watu milioni 6 katika eneo la Tigray walikuwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula katika mwezi wa Februari mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.