Pata taarifa kuu

Kenya, Congo-Brazzaville zatiliana saini mikataba 18 ya ushirikiano

Rais wa Kenya, William Ruto, mwishoni mwa juma lililopita, alihitimisha ziara yake nchini Congo Brazaville, ambako na mwenyeji wake rais Denis Sassou Nguesso, walitiliana saini mikataka karibu 18 ya ushirikiano ikiwemo ya utangamano na kiuchumi.

Kenya na Congo-Brazzaville zimetiliana saini mikataba ya ushirikiano
Kenya na Congo-Brazzaville zimetiliana saini mikataba ya ushirikiano © Wiliam Ruto
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, Ruto aligusia uwezekano wa kuanzisha tena safari za ndege kati ya Nairobi na Brazaville.

Aidha alipohutubia bunge, rais Ruto alitangaza nchi yake kuondoa vikwazo vya Viza kwa raia Congo wanaoingia nchini Kenya.

“Kama serikali ya Kenya tumeshafanya maamuzi kwamba raia wa Kongo Brazaville hamtahitaji viza kuingia nchini Kenya ni miongoni mwa sababu ambazo zinatuchochea kuongezeka kwa biashara kati ya nchi zetu.”alisema rais Ruto

Rais Ruto ameongeza kwamba watu wanapotangamana wanabadilishana mawazo pamoja na kujenga mahusiano, biashara na makampuni suala ambalo mataifa ya Afrika yanapaswa kufanya.

Mkataba mmoja ulitiwa saini wakati wa kikao cha wakuu hao wa nchi, na mengine 17 katika nyanja mbalimbali: kilimo, mifugo, mazingira, na utalii, viwanda vya madini na jiolojia, mafunzo ya kidiplomasia, kukuza vyama vya ushirika, miongoni mwa mengine.

Rais Ruto alieleza nia yake ya kuzindua upya shirika la ndege la Kenya Airways kati ya Nairobi na Brazzaville ifikapo mwisho wa mwaka. Shirika hilo la ndege lilisitisha hudumza zake katika mji mkuu wa Kongo miaka kadhaa iliyopita.

Kiongozi huyo wa Kenya pia alieleza kushtushwa na suala kwamba mataifa ya bara Afrika yenye mapato ya chini yanatumia asilimia 24 ya pato lao la taifa kwa malipo ya madeni, jambo ambalo linaleta changamoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.