Pata taarifa kuu

Mkutano wa kilele wa ECOWAS kufanyika Guinea-Bissau jumapili wiki hii

Nairobi – Guinea-Bissau itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa ECOWAS siku ya Jumapili, mkutano ambao unalenga kuangazia iwapo mabadiliko yanayoendelea nchini Mali, Burkina na Guinea yanakwenda kwa kasi ya kutosha kuelekea kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Rais wa Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, amabye pia ni rais wa ECOWAS .
Rais wa Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, amabye pia ni rais wa ECOWAS . © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kubwa ambalo lililopo mezani katika mkutano huo wa viongozi wa ECOWAS bila shaka ni lile la Mali. Ambapo hivi karibuni Mamlaka ya mpito ya Mali Juni 18, iliendehsa kura ya maoni ya kikatiba, kuashiria tarehe ya mwisho ya uchaguzi iliyokubaliwa na ECOWAS na, mbeleni, uchaguzi wa rais wa Februari 2024.

Lakini ucheleweshaji tayari umeonekana wakati uchaguzi wa viongozi wa tarafa ulipangwa kufanyika mwezi uliopita, haukufanyika na hakuna tarehe mpya iliyowasilishwa na Bamako.

Uchaguzi wa kura ya maoni umelalamikiwa na upinzani kwamba haukuwa huru na haki, huku baadhi ya waangalizi wakidai kwamba haukufanyika nchi nzima baada ya mji wa Kidal kutengwa kutokana na swala zima la usalama mdogo.

Kwa hivyo ECOWAS inajikuta katika hali tete, kwani italazimika kusema kama kura hii ya maoni ni hatua ya kusonga mbele au ni kikwazo cha kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Nchi zingine ambazo viongoozi hao wa ECOWAS wataangazia ni pmaoja na swala la usalama nchini BurkinFaso lakini pia Guinea Conakry ambayo utawala wa mpito unaelekea kwenye tamati desemba mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.