Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Vifaa vya kijeshi vya Misri vyatumwa Niger

Niger imepokea siku ya Ijumaa silaha nzito na magari ya kivita, yaliyotolewa na Misri kusaidia nchi hii maskini ya Saheli kupambana na makundi ya kijihadi, ambayo mashambulizi yao yanadhoofisha mashariki na magharibi mwa nchi, imetangaza wizara ya usalama ya Niger.

Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, inakabiliwa kwenye mipaka yake sita kati ya saba na majambazi wenye silaha au makundi ya kijihadi.
Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, inakabiliwa kwenye mipaka yake sita kati ya saba na majambazi wenye silaha au makundi ya kijihadi. AFP - BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

Hasa, magari 30 ya kivita (upelelezi) ya aina ya BRDM-2, karibu mizinga ishirini na bunduki 122mm, bastola zaidi ya 2,000 na bunduki za kushambulia za AK47, pamoja na risasi, zilipokelewa huko Niamey na viongozi wa jeshi la Niger.

Alkassoum Indatou, Waziri wa Ulinzi wa Niger, amepongeza "ishara hii muhimu sana" kutoka Misri, ambayo "bado inaonyesha mshikamano wake" nchini Niger "katika mazingira magumu hasa ya usalama" katika Sahel.

Misri pia inafunza kikosi maalum cha jeshi la Niger, amebainisha Bw. Indatou, wakati wa hafla mbele ya balozi wa Misri nchini Niger.

Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, inakabiliwa katika mipaka yake sita kati ya saba na majambazi wenye silaha au makundi ya kijihadi, kama vile Boko Haram kutoka Nigeria naIslamic State katika Afrika Magharibi (ISWAP) huko mashariki, na makundi mengine ya kijihadi yanayohusishwa na Al-Qaeda na Islamic State katika Grand Sahara (EIGS) magharibi.

Katika mapambano yake dhidi ya wanajihadi, Niger inafurahia uungwaji mkono wa nchi kadhaa za Magharibi zikiwemo Ufaransa na Marekani, ambazo zina kambi za kijeshi huko. Wanajeshi 1,500 wa Ufaransa wapo nchini humo.

Aidha, EU ilitangaza siku ya Jumatano kuimarisha uungaji mkono wake wa kijeshi ili kupambana na makundi ya kijihadi. Niger "itakuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika" kunufaika na msaada wa Ulaya kuvipa vikosi vyake "vifaa vya kuua", hasa "risasi za kisasa kwa helikopta za kivita", ametangaza Josep Borrell, mkuu wa diplomasia ya Umoja wa Ulaya anayezuru Niamey.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.