Pata taarifa kuu

Mataifa 12 ya Afrika kunufaika na chanjo ya malaria: WHO

Nairobi – Shirika la afya duniani (WHO) na washirika wake linasema karibia dozi milioni 18 za kwanza za chanjo dhidi ya malaria zitapelekwa katika mataifa 12 ya bara Afrika kufikia mwaka wa 2025.

Kenya, Ghana na Malawi ni miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kunufaika na mpango huo
Kenya, Ghana na Malawi ni miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kunufaika na mpango huo © Baz Ratner / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kupata chanjo hiyo ni pamoja na Malawi, Ghana na Kenya, ambako tayari chanjo ya Mosquirix imetumika kufanya majaribio.

Kutokana na idadi ya uhitaji wa chanjo, kipau mbele kitaelekwa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na ambapo zitatumika kikamilifu.

Msumbiji na Sudan zimetengwa kwa sababu ya viwango vyao vya juu vya kuachana na matumizi ya chanjo.

WHO inasema chanjo hiyo - iliyotengenezwa na kampuni ya Uingereza ya GSK - inaweza kuokoa maisha ya mtu mmoja kwa kila watoto 200 wanaochanjwa.

Malaria huua takriban watoto nusu milioni wa Kiafrika chini ya miaka mitano kila mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.