Pata taarifa kuu

Ghana: Bunge linataka kupitishwa kwa sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Nairobi – Bunge nchini Ghana, limeunga mkono mapendekezo ya kufanyika kwa marekebisho kuhusu muswada unaopendekeza wapenzi wa jinsia moja kufungwa jela miaka mitatu.

Tayari mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Ghana
Tayari mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Ghana AP - Francisco Seco
Matangazo ya kibiashara

Aidha wakereketwa wa haki za wapenzi wa jinsia moja LGBT wanaweza kufungwa jela kwa kipindi cha miaka kumi.

Mapendekezo hayo ambayo yameungwa mkono na wabunge, yanatarajiwa kufanywa tathmini zaidi kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria. Tayari mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Ghana.

Hatua hiyo ya bunge imekashifiwa ndani na nje ya taifa hilo, wakosoaji wa sheria hiyo wakieleza kwamba inakiuka haki za watu kama ilivyo kwenye katiba.

Licha ya kukashifiwa vikali, baadhi ya wanaounga mkono hatua hiyo ya bunge la Ghana wanahisi kuwa itarejesha maadili nchini humo.

Tayari wanaopinga muswada huo wanasema kuwa watawasilisha kesi mahakamani kuupinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.