Pata taarifa kuu

Ethiopia: Wakuu wa polisi wameuawa katika jimbo la Amhara

Nairobi – Watu wasiojulikana wameuawa maofisa watatu wa ngazi ya juu katika eneo linalokabiliwa na utovu wa usalama la Amhara nchini Ethiopia kwa mujibu wa mamlaka katika eneo hilo.

Wapiganaji wa  Amhara walisaidia serikali ya Ethiopia kupigana dhidi ya TPLF
Wapiganaji wa Amhara walisaidia serikali ya Ethiopia kupigana dhidi ya TPLF AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Jimbo la Amhara limekuwa likabiliwa na machafuko tangu serikali ya shirikisho mapema mwaka huu kutangaza kuvunja vitengo vya wanajeshi wa kimaeneo na kuwajumuisha katika jeshi la kitaifa na maofisa wa polisi wa majimbo.

Mkuu wa polisi na kiongozi wa kitengo cha kuzuia uhalifu katika wilaya ya Dejen kusini mwa Amhara waliauwa na dereva kujeruhiwa katika shambulio hilo la Jumatatu.

Jumanne ya wiki hii, mkuu wa polisi katika mji wa Shewa Robit aliuawa kwa mujibu wa taarifa ya meya wa eneo hilo kwenye mtandao wa facebook ambayo haikutoa maelezo zaidi.

Mamlaka imetangaza makataa ya watu kutembea nje kuanzia saa kumi na mbili jioni katika mji wa Shewa Robit, unaopatikana mashariki mwa mji wa Dejen, ikiwa ni umbali wa kilomita 200 kutoka jiji kuu la Addis Ababa.

Hadi tukichapisha taarifa hii, hakuna kundi lililokuwa limekiri kuhusika na mauji hayo.

Wanajeshi maalum kutoka katika eneo la Amhara waliwasaidia wanajeshi wa serikali ya Ethiopia kupigana dhidi ya wapiganaji wa TPLF ambao walikuwa wameanzisha uasi dhidi ya serikali ya waziri mkuu Abiy Ahamed mwaka wa 2020.

Machafuko nchini Ethiopia kati ya TPFL na serikali ya shirikisho yamalizika mwezi Novemba mwaka jana baada ya pande husika kutia saini makubaliano ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.