Pata taarifa kuu

Sudan: Kiongozi wa RSF Hamdane Daglo yuko wapi?

Nairobi – Nchini Sudan, wakati huu wanajeshi na wanagambo wa RSF wanapoendelea kukabiliana jijini Khartoum, vita ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu Elfu tatu, Jenerali Mohamed Hamdane Daglo maarufu kama Hemedti, kiongozi wa RSF hajasikika wala kuonekana, je yuko wapi?

Generali Mohammed Hamdan Daglo, Kongozi wa RSF nchini Sudan
Generali Mohammed Hamdan Daglo, Kongozi wa RSF nchini Sudan © capture d'écran/lemonde.fr/afrique
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa RSF hajaonekana kwa siku zaidi ya 40. Jenerali, Hemedti, hajawasiliana kupitia vyombo vya Habari au hata mitandao ya kijamii, kama ilivyokuwa mwanzoni mwa vita hivi, katikati ya mwezi Aprili.

Kumekuwa na maswali kuhusu aliko kiongozi huyo wa wanamgambo hao wa RSF, baada ya Mei 30 kaka yake Abderrahim Dagelo alipojitokeza jijini Khartoum na kuthibitisha kuwa Hemedti yupo kwenye hali nzuri ya kiafya na anaendelea na majukumu yake ya kuongoza RSF.

Hata hivyo, Mei 15 kupitia ujumbe wa sauti, Mohamad Hamdane Dagelo alituma ujumbe wa sauti akisema yupo pamoja na wapiganaji wake jijini Khartoum , lakini pia Juni 28 alituma ujumbe mwingine wa sauti akiwatakia raia wa Sudan akiwatakia sikukuu ya Eid el Adha.

Ripoti zinasema, kiongozi huyo wa RSF alitembelea mjini  Benghazi nchini Libya na kukutana na kiongozi wa eneo hilo Khalifa Haftar mwezi mmoja uliopita, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa kuhusu aliko Jenerali Daglo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.