Pata taarifa kuu

Baraza la Ulaya launga mkono Afrika kuwania kwa G20

Katika hafla ya mkutano wa kilele wa 27 ambao unafanyika huko Brussels, Baraza la Ulaya limetoa uungaji mkono wake kwa kugombea kwa Umoja wa Afrika kwa kundi la nchi zizostawi kiviwanda, G20.

Rais Macky Sall, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa mkutano wa kilele na Umoja wa Ulaya, alikuwa mmoja wa wasemaji walioonekana zaidi wa kampeni hii ya kupendelea kiti cha Afrika, na Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini, nchi pekee ya Afrika ambayo ni mwanachama kamili wa G20.
Rais Macky Sall, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa mkutano wa kilele na Umoja wa Ulaya, alikuwa mmoja wa wasemaji walioonekana zaidi wa kampeni hii ya kupendelea kiti cha Afrika, na Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini, nchi pekee ya Afrika ambayo ni mwanachama kamili wa G20. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet

"Ninashukuru kwa moyo mkunjufu nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, EU, kufuatia uamuzi wa pamoja wa Baraza la Ulaya kuunga mkono ugombea wa Afrika kwa kundi la G20," Macky Sall aliandika siku ya Ijumaa.

Ni hatua ya matokeo kwa safari ya Afrika kuelekea G20, ugombea ulitangazwa kwa msisitizo zaidi na zaidi kwa mwaka mmoja na nusu na ambao unaonekana kupata msukumo mpya na ufadhili huu wa Umoja wa Ulaya. Kama katika mikutano yao yote ya kilele, nchi za Umoja wa Ulaya zilipitisha rasmi seti ya mahitimisho ya pamoja na katika aya ya 40 kunapatikana uamuzi huu wa Umoja wa Ulaya kwa kuiunga mkono Afrika.

"Kwa mujibu wa ahadi za ushirikiano wa pande nyingi zilizotolewa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wa tarehe 17 na 18 Februari 2022, Baraza la Ulaya linaunga mkono uwepo wa Umoja wa Afrika katika majukwaa ya kimataifa, hususan ndani ya G20".

Msimamo wa Ulaya kwa hiyo sasa umeundwa ipasavyo na inatokana na ahadi ambazo Ufaransa ilirejelea wakati wa ziara ya rais wa Senegal huko Paris mwezi wa Februari.

Rais Macky Sall, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa mkutano wa kilele na Umoja wa Ulaya, alikuwa mmoja wa wasemaji walioonekana zaidi wa kampeni hii ya kupendelea kiti cha Afrika, na Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini, nchi pekee ya Afrika ambayo ni mwanachama kamili wa G20.

Umoja wa Ulaya una makao yake makuu na una nchi tatu wanachama, Ufaransa, Italia na Ujerumani. Nchi hizi tatu zenye nguvu za Ulaya zinaweza kusaidia kuwashawishi wanachama wengine wa G20 juu ya hitaji la usawazishaji huu, ambao Marekani pia inaunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.