Pata taarifa kuu

Mwili wa kijana wa Guinea aliyeuawa na afisa wa polisi wa Ufaransa warejeshwa nyumbani

Mwili wa kijana mwenye umri wa miaka 19 kutoka Guinea aliyeuawa wakati wa ukaguzi wa magari barabarani mnamo Juni 14 kusini magharibi mwa Ufaransa ulipokelewa Jumatano jioni huko Conakry na familia yake na mamlaka ambayo ilitaka haki itendeke, mwandishi wa habari wa AFP alishuhudia.

Mnamo Juni 14 karibu na Angoulême, Alhoussein Camara aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kukamatwa.
Mnamo Juni 14 karibu na Angoulême, Alhoussein Camara aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kukamatwa. AFP - THIBAUD MORITZ
Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa huzuni mkubwa tunapokea mwili wa kijana Alhoussein. Mkuu wa Nchi aliahidi kuwa mwili huo utarejeshwa nchini Guinea ili kufanyike maziko ya heshima, ambayo yanafanywa kwa neema ya Mungu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea, Morissanda Kouyaté, alisema alipowasili katika uwanja wa ndege.

Mazingira ya kifo cha  Alhoussein yatafafanuliwa. Guinea inataka mahakama kufanya kazi yake yote nchini Ufaransa, kufafanua mazngira ya kifo chake", aliongeza. "Ni mpendwa wetu ambaye ametoka tu, mtoto kipenzi", alisema baba wa kijana aliyeuawa, Fodé Camara, ambaye aliwashukuru viongozi serikalini kwa kuwa karibu na familia hiyo.

Afisa wa Polisi wa Ufaransa, mwenye umri wa miaka 52, aliyemuua kwa risasi kijana huyo alishtakiwa Jumatano kwa mauaji ya kukusudia, "na kupigwa marufuku kumiliki silaha na marufuku ya kufanya tena kazi yake", alitangaza mwendesha mashtaka wa umma wa Angoulême.

Mapema asubuhi ya Juni 14, huko Saint-Yrieix-sur-Charente, katika viunga vya Angoulême, Alhoussein Camara aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi alipokuwa akijaribu kutoroka kukamatwa wakati wa ukaguzi wa magari barabarani. 

Kati ya watu 800 na 1,000 walishiriki maandamano baada ya kifo chake, wakitaka haki itendeke, akishiriki maandamano hayo balozi wa Guinea nchini Ufaransa, Sinkoun Sylla. Kesi hii inaangazia kifo cha Jumanne huko Nanterre, karibu na Paris, cha Nahel, dereva kijana mwenye umri wa miaka 17, aliyeuawa na afisa wa polisi wakati aalipokuwa akijaribu kutoroka ukaguzi wa magari barabarani. Mkasa huo ulisababisha ghasia za usiku kwa siku mbili mfululizo kote Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.