Pata taarifa kuu

Morocco yamwagiza balozi wake kurejea nyumbani baada ya sakata la uchomaji wa Koran

Nairobi – Morocco inamwita nyumbani balozi wake nchini Uswidi kufuatia kuchomwa kwa Koran kwenye maandamano mjini Stockholm.

Salwan Momik - anachunguzwa kwa uchochezi wa chuki
Salwan Momik - anachunguzwa kwa uchochezi wa chuki AFP - JONATHAN NACKSTRAND
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mashauri ya Kigeni mjini Rabat ilitaja hatua hiyo kuwa ya kuudhi na kutowajibika wakati Waislamu walikuwa wakisherehekea mojawapo ya siku takatifu zaidi katika kalenda yao.

Mratibu wa maandamano hayo - ambaye anasemekana kuwa mzaliwa wa Iraq Salwan Momik - anachunguzwa kwa uchochezi wa chuki.

Mahakama ya Uswidi ilikuwa imeamua maandamano hayo yaruhusiwe kuendelea kwa misingi ya uhuru wa kujieleza.

Maofisa kutoka katika baadhi ya mataifa ikiwemo Mashariki ya kati, Marekani, Misiri na Jordan wamelaani kitendo hicho cha uchomaji wa Koran wakati wa maandamano hayo yalioidhinishwa na maofisa wa polisi.

Salwan Momika, mwenye umri wa miaka 37 aliyehamia nchini Uswidi miaka kadhaa iliyopita akitokea nchini Iraq, alitekeleza kitendo hicho wakati waumini wa kiisilamu wakisherekea siku kuu ya al-Adha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.