Pata taarifa kuu

Nigeria: Msafara mrefu wa magari ya Tinubu waghadhabisha raia

Nairobi – Raia mjini Lagos nchini Nigeria, wameonekana kukasirishwa baada ya kuwasili kwa Rais Bola Tinubu katika jiji hilo Jumanne jioni akiwa na msafara mrefu wa magari.

Bola Tinubu, Rais wa Nigeria
Bola Tinubu, Rais wa Nigeria AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia walisema kiongozi aliandamana na zaidi ya magari 100 alipokuwa akirejea kutoka Uingereza kwa ajili ya likizo ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Kwa mujibu wa video zilizochapishwa kwenye mitadao ya kijamii, magari hayo makubwa makubwa yameonekana yakisindikizwa na maofisa wa jeshi wakati barabara zikiwa zimefungwa kwa matumizi ya raia.

Raia wa Nigeria wanahisi kuwa tukio hilo ni ubadirifu wa fedha za umma haswa wakati huu ambapo mataifa mengi ya bara ya Afrika yanakabiliwa na changamoto za kiuchumi na mfumuko wa bei za bidhaa.

Tinubu alichukuwa hatamu ya kuongoza taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kutoka kwa mtangulizi wake Muhamadu Buhari mwezi uliopita.

Wapinzani nchini humo walipinga ushindi wa Tinubu kwa misingi kuwa haukuzingatia uwazi wakisema kwamba kulikuwepo na wizi wa kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.