Pata taarifa kuu

Sudan : Mapigano yamesababisha watu zaidi ya laki 2 kuyahama makazi yao

NAIROBI – Zaidi ya watu milioni 2 na laki 5 wamelazimishwa kukimbia makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea nchini Sudan, wakati huu ripoti za miili kutapakaa kwenye jimbo la Darfur Magharibi, zikizidisha wasiwasi.

Watu zaidi ya laki mbili wameripotiwa kuyahama makazi yao mapigano yakiendelea
Watu zaidi ya laki mbili wameripotiwa kuyahama makazi yao mapigano yakiendelea AP - Peter Louis
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii ya umoja wa Mataifa inatolewa wakati ambapo muda wa siku tatu wa usitishaji mapigano ukitarajiwa kutamatika hivi leo, huku kukiwa hakuna matumaini ikiwa viongozi wanaohasimiana watakubali kuongeza muda.

Aidha wakati huu muda wa kusitisha mapigano ukielekea ukiongoni, raia kwenye mji wa Khartoum, wameripoti makabiliano makali katika baadhi ya maeneo kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa RSF.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, watu zaidi ya elfu 1 wameuawa katika mji wa Geneina peke yake, huku umoja wa Mataifa wenyewe ukisema watu elfu 2 wameuawa kiujumla tangu kuanza kwa mapigano mwezi April.

Haya yanajiri wakati huu tume za haki za binadami ya umoja wa Mataifa, ikionya kuhusu kutekelezwa kwa vitendo vya uhalifu wa kivita, mauaji na ubakaji kwenye eneo la Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.