Pata taarifa kuu

Watu 17 wameuawa Kusini mwa Khartoum katika shambulio la ndege za kivita

NAIROBI – Watu 17 wameuawa Kusini mwa jijini la Khartoum, baada ya kushambuliwa na ndege za kivita, katika mapiganano yanayoendelea kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa RSF.

Mapigano yamendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa kwa vita
Mapigano yamendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa kwa vita © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa afya wamesema, miongoni mwa watu hao 17 waliopoteza maisha ni watoto watano kufuatia shambulio hilo lilitokea leo Jumamosi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, idara ya afya imesema, milipuko hiyo imeshuhudiwa katika Wilaya ya Yarmouk, na mbali na mauaji, watu wengine wamejeruhiwa.

Wiki hii, vita kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF, yaliingia katika mwezi wa tatu, ambapo yamebabisha zaidi ya watu Elfu mbili kupoteza maisha na wengine zaidi ya Milioni 2.2 wameyakimbia makwao wakiwemo 528,000 kukimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia wahamiaji-IOM.

Jumuiya ya IGAD imetangaza mpango wa kukutana ana kwa ana na Majenerali nchini humo, ili kujaribu kupata suluhu lakini upande jeshi umekataa uongozi wa rais wa Kenya William Ruto kutafuta mwafaka, kwa madai kuwa anaegemea upande mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.