Nigeria: Rais Tinubu amemfuta kazi mkuu wa tume ya kupambana na rushwa
NAIROBI – Rais mpya wa Nigeria Bola Tinubu amemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana mkuu wa Tume ya kupambana na rushwa nchini humo, Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC).
Imechapishwa:
Abdulrasheed Bawa alitakiwa kuondoka katika wadhifa huo ili kuruhusu uchunguzi sahihi kuhusu harakati zake wakati akiwa madarakani".
Ingawa ni jambo la kawaida kwa mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi kuondolewa mara tu rais mpya anapoingia madarakani, taarifa ya serikali ilisema kusimamishwa huko kulifuatia tuhuma nzito kuhusiana na matumizi mabaya ya ofisi yanayomkabili.
Afisa huyo mwenye umri wa 43 amekuwa akikabiliwa na tuhuma za ufisadi tangu alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa EFCC mnamo 2021, jambo ambalo amekanusha.
Katika mahojiano na BBC Hausa mwezi uliopita, gavana wa zamani wa jimbo la kaskazini la Zamfara alimshutumu Bawa kwa madai ya kudai hongo ya $2m (£1.58m) kutoka kwake. Alikanusha madai hayo.
Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 150 kati ya nchi 180 katika mtizamo wa shirika la Transparency International kuhusu ufisadi.