Pata taarifa kuu

Ethiopia yakosoa hatua ya mashirika ya misaada kusitisha huduma zake

NAIROBI – Serikali ya Ethiopia imekosoa hatua ya mashirika ya misaada kusitisha huduma zake kwa raia wa taifa hilo.

Ethiopia yasikitishwa na hatua ya usitishwaji wa utoaji wa chakula cha msaada
Ethiopia yasikitishwa na hatua ya usitishwaji wa utoaji wa chakula cha msaada Getty Images - J. Countess
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Legesse Tulu, amesema hatua ya mashirika ya  misaaada USAID na lile la mpango wa chakula duniani WFP, kusitisha kutoa huduma zake kwa raia wa Ethiopia ni kama adabu kwa mamilioni ya raia wa taifa hilo ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea misaada.

Tulu ameongeza kuwa hatua ya masharika hayo hata hivyo ni ya kisiasa hasa kutokana kwamba yanatuhumu serikali kwa kuhusika kuelekeza chakula cha misaada kuuzwa kwa masoko nchini humo .

Mwezi uliopita USAID na WFP zilisitisha misaada ya  chakula kwa taifa la Ethiopia kwa kile mashirika hayo mawili yalidai kuwa chakula hicho hakijakuwa kikiwafikia wahusika na badala yake kimekuwa kikiuzwa katika masoko ya Ethiopia.

Ni hatua ambayo inatarajiwa kuathiri zaidi ya watu milioni 20  ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wametegemea chakula hicho kutokana na athari ya vita katika jimbo la Tigray na ukame ambao kwa muda umeathiri eneo la Kusini na kusini magharibi mwa Ethiopia.

Licha ya tetesi za chakula cha misaada kuuzwa kwa masoko hakuna aliyekamtwa kuhusiana na tuhuma hizo, wakati huu taifa hilo likiendelea kupokea wakimbizi wanaokimbia vita nchini Suda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.