Pata taarifa kuu

CAR: Askari 60 wa Tanzania warejeshwa makwao baada ya kushtumiwa unyanyasaji wa kingono

Umoja wa Mataifa utawarejesha nyumbani wanajeshi wote 60 wa kitengo cha jeshi la Tanzania katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), baada ya "tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia" zinazowakabili wanajeshi11 kati yao, kulingana na taarifa kutoka MINUSCA kwa shirika la habari la AFP. 

Wanajeshi wa MINUSCA wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wanajeshi wa MINUSCA wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ushahidi wa awali uliokusanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Uangalizi wa Ndani (OIOS) ulifichua kuwa wanajeshi 11 wa kitengo hicho, waliopelekwa katika kambi ya muda ya MINUSCA magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanahusika katika unyonyaji na unyanyasaji wa kingono kwa waathiriwa wanne", inabainisha MINUSCA, bila kutoa maelezo juu ya tarehe ya tukio. Waathiriwa "walipokea huduma ya haraka na usaidizi kupitia washirika wa misheni, kulingana na mahitaji yao ya matibabu, kisaikolojia na ulinzi", kinaongeza chanzo kimoja.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ulifanya uchunguzi wa ndani "kutathmini tuhuma hizo, kuwatambua na kuwasikiliza wanaodaiwa kuwa waathiriwa", na kuongeza kuwa "imeziarifu mamlaka za Tanzania kuhusu tuhuma hizo" ambao "walibaini uzito wa tuhuma hizo na kuchukua hatua zinazohitajika". 

Shutuma za unyanyasaji wa kingono unaofanywa na walinda amani duniani kote ni kitendo kinachojirudi, hasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kitendo ambachoo Umoja wa Mataifa umekuwa ukijaribu kukabiliana nacho kwa miaka mingi. Mnamo 2021, Umoja wa Mataifa uliamuru kuondolewa kwa wanajeshi 450 wa Gabon kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia na ambapo serikali ya Libreville ilifungua uchunguzi.

Kisha MINUSCA ilianzisha "kesi nyingi za madai ya unyanyasaji wa kingono kushughulikiwa" kwa "wasichana watano", katika eneo moja katikati mwa nchi. Tangu mwaka wa 2015, Umoja wa Mataifa umeonyesha kwenye tovuti yake kwamba imerekodi shutuma 254 za unyanyasaji wa kingono zikiwalenga wanajeshi wa MINUSCA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na imewatambua waathiriwa 659.

Vita mbaya vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka mwaka wa 2013 wakati muungano wa waasi wenye Waislamu wengi, Séleka, ulipompindua Rais François Bozize. Bozize kwa upande wake aliwahamasisha hasa wanamgambo wa kujilinda wa Kikristo, anti-balakas, kujaribu kurejesha mamlaka.

Maelfu ya raia waliuawa kwa umati hadi kilele cha vita mwaka 2016 na Umoja wa Mataifa ulishutumu Seleka na anti-balaka kwa uhalifu dhidi ya binadamu, licha ya kuwepo kwa kikosi kikubwa cha kulinda amani cha walinda amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.