Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mapigano yarindima kati ya jeshi la Chad na waasi, ripoti zakinzana

Mapigano ya wiki moja yaliripotiwa kati ya jeshi na waasi kaskazini mwa Chad, ambapo jeshi lilidai siku ya Jumatano kuwaua waasi 23, huku waasi wakidai kuua wanajeshi 15, katika milima ya Tibesti ambapo kambi hizo mbili hupigana mara kwa mara.

Mnamo Mei 31, jeshi lilidai kushambulia "safu" ya waasi wa FNDJT na wale wa kundi la CCMSR katika jimbo la Kouri Bougoudi.
Mnamo Mei 31, jeshi lilidai kushambulia "safu" ya waasi wa FNDJT na wale wa kundi la CCMSR katika jimbo la Kouri Bougoudi. © Carol Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika eneo hili la jangwa, makundi makuu ya waasi wa Chad, yanayoendesha harakazi zao kwa muda mrefu kusini mwa nchi jirani ya Libya, wanaendelea kujizatiti ambapo wanawakabilia wanajeshi na walianzisha mashambulizi katika msimu wa masika wa mwaka 2021 ambapo walimuua Rais Idriss Déby Itno alikwenda vita.

Mnamo Mei 31, jeshi lilidai kushambulia "safu" ya waasi wa FNDJT na wale wa kundi la CCMSR katika jimbo la Kouri Bougoudi.

Tangu wakati huo, na hasa mwishoni mwa "operesheni za kijeshi" siku ya Jumatatu na Jumanne, "idadi ya mwisho ni waasi 23 waliouawa na wanane kujeruhiwa katika safu yetu", msemaji wa jeshi Jenerali Azem Bermandoa Agouna ameliamia shirika la habari la AFP. kKwa upande wake kundi la waasi la FNDJT, lilihakikisha siku ya Jumanne katika taarifa kwa vyombo vya habari  liliua "wanajeshi 15 wakiwemo maafisa wakuu wawili".

Ripoti zilizotolewa na kambi hizo mbili wakati wa mapigano yao hazijabitishwa na chanzo huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.