Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Israel kushiriki mazoezi nchini Morocco kwa mara ya kwanza

Wanajeshi wa Israel watashiriki "kikamilifu" kwa mara ya kwanza katika mazoezi ya kijeshi katika ardhi ya Morocco, mazoezi ya kimataifa "African Lion 2023", ambayo ni makubwa zaidi katika bara la Afrika, ambayo yanaanza Jumanne, kulingana na jeshi la Israel.

Israel tayari ilishiriki katika "Simba wa Kiafrika" mwaka jana lakini tu katika ngazi ya waangalizi wa kijeshi wa kimataifa, bila kupeleka askari.
Israel tayari ilishiriki katika "Simba wa Kiafrika" mwaka jana lakini tu katika ngazi ya waangalizi wa kijeshi wa kimataifa, bila kupeleka askari. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

"Ujumbe wa wanajeshi na makamanda 12 kutoka Kikosi cha Upelelezi cha Golani waliondoka siku ya Jumapili (Israel) kwa ajili ya mazoezi ya 'Simba wa Afrika 2023' nchini Morocco," nchi mwenyeji Israel imesema katika taarifa iliyotolewa Jumatatu. "Hii ni mara ya kwanza kwa jeshi la Israel kushiriki kikamilifu katika mazoezi haya ya kimataifa katika ardhi ya Morocco," imesema taarifa hiyo.

Brigedi ya Golani ni kitengo cha wanajeshi wasomi wa kikosi cha nchi kavu, kinachojishughulisha mara kwa mara katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kimabavu. Toleo la 19 la zoezi la "Simba wa Afrika" lialoandaliwa kwa pamoja na Morocco na Marekani, litafanyika hadi Juni 16 na litajumuisha karibu wanajeshi 8,000 kutoka nchi 18.

"Kwa muda wa wiki mbili zijazo, wanajeshi wetu watazingatia mafunzo katika hali tofauti za mapigano ambayo yataambatanisha vita vya msituni, mijini na vita vya chini ya ardhi, na hivyo kuhitimisha kwa mazoezi ya pamoja kwa majeshi yote yanayoshiriki," taarifa ya jeshi la Israel imesema.

Israel tayari ilishiriki katika "Simba wa Kiafrika" mwaka jana lakini tu katika ngazi ya waangalizi wa kijeshi wa kimataifa, bila kupeleka askari uwajani.

Kulingana na makao makuu ya Kikosi cha Wanajeshi wa Kifalme wa Morocco (FAR), mazoezi haya ya kila mwaka yatafanyika katika mikoa saba ya nchi hii. Yanajumuisha mazoezi ya kupanga uendeshaji na mapambano dhidi ya silaha za maangamizi makubwa, mazoezi ya kimbinu ardhini, baharini, angani na mafunzo ya vikosi maalum, pamoja na shughuli za anga, kulingana na FAR.

Morocco na Israel zimekuwa zikifanya kazi ya kuharakisha ushirikiano wao - kijeshi, usalama, biashara na utalii - tangu kurejeshwa kwa uhusiano wao mnamo mwezi Desemba 2020, ndani ya mfumo wa Mkataba wa Abraham, mchakato kati ya serikali ya Kiyahudi na nchi kadhaa za Kiarabu na Washington. Kwa upande wake, Rabat ilipata kutoka Washington kutambuliwa kwa "uhuru wa Morocco" katika eneo la Sahara Magharibi dhidi ya watu wanaojitenga wa Polisario Front inayoungwa mkono na Algiers.

Baada ya Waziri wa Uchukuzi wa Israel Miri Regev, Spika wa Bunge la Israel (Knesset) Amir Ohana anatarajiwa nchini Morocco siku ya Jumatano kwa ziara rasmi ya "kihistoria", ya kwanza kufanywa na mspika wa bunge la Israel, kwa mwaliko wa mwenzake Rachid Talbi El Alami. Bw. Ohana, Waziri wa zamani wa Usalama wa Ndani wa Israel na mwanachama wa Likud, chama cha mrengo wa kulia cha Benjamin Netanyahu, ana asili ya Morocco.

Hata hivyo, maelewano ya pande zote kati ya nchi hizo mbili washirika yanakuja dhidi ya, angalau kwa maoni ya umma, kuingia kwa mamlaka katika Israeli ya mikondo ya kitaifa yenye uhasama wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo na Wapalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.