Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-KAZI

Morocco: Muungano wa wafanyakazi waandamana dhidi ya gharama kubwa ya maisha

Mamia ya wanaharakati kutoka chama cha wafanyakazi nchini Morocco wameandama Jumapili huko Casablanca, magharibi mwa Morocco, wakipinga kile walichokiita "gharama kubwa ya maisha" na "kutochukua hatua kwa serikali", licha ya kupigwa marufuku kwa maandamano hayo. Wakitoka kote nchini, wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi kutoka Shirikisho la Wafanyakazi wa Kidemokrasia (CDT, kushoto) walikusanyika katika kituo cha kihistoria cha mji mkuu wa kiuchumi.

Maandamano huko Casablanca, Morocco, kufuatia wito wa Shirikisho la Wafanyakazi kupinga gharama ya juu ya maisha na kudai nyongeza ya mishahara, Juni 4, 2023.
Maandamano huko Casablanca, Morocco, kufuatia wito wa Shirikisho la Wafanyakazi kupinga gharama ya juu ya maisha na kudai nyongeza ya mishahara, Juni 4, 2023. © AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya wafanyakazi vinashutumu makubaliano ya kijamii yaliyohitimishwa mwaka jana lakini hayakutumika.

"Tuko hapa kulialia kutoridhika kwetu na kupanda kwa bei na mashambulizi dhidi ya ununuzi," ameeleza Abdellah Lagbouri, aliyekuja kujiunga na wenzake kutoka Agadir (kusini) hadi Casablanca na ni mwanachama wa CDT. "Ni aibu, riziki ya wafanyakazi iko hatarini," walipinga waandamanaji. “Watu wenye mapato ya chini wanawezaje kuishi? kwa hali hii ya kupanda kwa bei za vyakula, wamesema.

Hapo awali, CDT ilitaka kufanya maandamano ya kitaifa huko Casablanca lakini maandamano hayo yalipigwa marufuku na mamlaka za mitaa, amesema Tarik Alaoui El Housseini, mjumbe wa Baraza la Kitaifa la CDT. "Tumeamua kususia kazi," ameleza. Maandamano hayo yalifanyika bila ya tukio kubwa, lakini yalisababisha makabiliano machache tu na polisi, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.