Pata taarifa kuu
HAKI-USALAMA

Libya: Wanachama 23 wa IS wahukumiwa kifo

Wanajihadi 23 waliopatikana na hatia ya kupigania kundi la Islamic State (IS) wamehukumiwa kifo siku ya Jumatatu na mahakama nchini Libya, kulingana na chanzo cha mahakama. Wengine kumi na wanne wamehukumiwa kifungo cha maisha, kulingana na chanzo hicho.

IS iliiteka Sirte mnamo mwezi Juni 2015, ikitumia fursa ya machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mnamo 2011 baada ya raia kushika silaha. Wakati wa mashambulizi yao, vikosi vya ndani vilinufaika kutokana na msaada wa jeshi la Marekani ambalo lilikuwa limekusanya ndege zisizo na rubani, meli za kivita na ndege za kivita hadi kutwaa tena mji huo.
IS iliiteka Sirte mnamo mwezi Juni 2015, ikitumia fursa ya machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mnamo 2011 baada ya raia kushika silaha. Wakati wa mashambulizi yao, vikosi vya ndani vilinufaika kutokana na msaada wa jeshi la Marekani ambalo lilikuwa limekusanya ndege zisizo na rubani, meli za kivita na ndege za kivita hadi kutwaa tena mji huo. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hizo zimetolewa na mahakama ya Misrata (mashariki), mji ambao wengi wa wapiganaji waliuawa wakati wa mashambulizi dhidi ya IS yaliyolenga kuwaondoa wapiganaji wa kijihadi kutoka Sirte, ngome yake kaskazini mwa Libya mnamo mwaka 2015 na 2016.

Wakati wa kesi hii, iliyofunguliwa mwezi Agosti 2022, watoto watatu pia wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani, wakili Lotfi Mohaychem, anayewakilisha familia ya watu waliouawa wakipambana dhidi ya IS, ameliambia shirika la habari la AFP baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo. Kwa jumla, karibu wanajihadi hamsini walipatikana na hatia ya mauaji na kuwa na uhusiano na kundi hili la kigaidi, kulingana na chanzo cha mahakama.

Wakiwa wamepandishwa kizimbani, wakiwa wamevalia sare za bluu, wakiwa wamenyolewa vichwa na ndevu, washtakiwa hao walionekana kwenye chumba kilichojaa watu, ambapo familia za watu waliouawa wakati wa vita vya ukombozi wa Sirte zilikuwepo. Watuhumiwa hao kutoka Libya, Sudan au Palestina, walikamatwa mwezi Desemba 2016, baada ya kutekwa kwa Sirte, mji wa pwani ulio kilomita 450 kutoka Tripoli.

Kama mawakili wa familia za waathiriwa, tunaona uamuzi wa mahakama kuwa wa kuridhisha na wa haki(...) Mahakama imewahukumu wale ambao hatia yao ilithibitishwa na kuwaachilia wale ambao hapaklupatikana ushahidi wa kutosha," Mohaychem amesema.

Hukumu hizo ziliposomwa, wanawake kadhaa walionyesha furaha yao, huku kukiwa na nderemo na vifijo, wakiimba “Mungu ni Mkuu” na “damu ya mashahidi haijamwagika bure”. 

IS iliiteka Sirte mnamo mwezi Juni 2015, ikitumia fursa ya machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa dikteta Muammar Gaddafi mnamo 2011 baada ya raia kushika silaha. Wakati wa mashambulizi yao, vikosi vya ndani vilinufaika kutokana na msaada wa jeshi la Marekani ambalo lilikuwa limekusanya ndege zisizo na rubani, meli za kivita na ndege za kivita hadi kutwaa tena mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.