Pata taarifa kuu

Mkataba wa usitishaji wa mapigano kuaanza leo Jumatatu nchini Sudan

NAIROBI – Wakati ambapo leo hii pande zinazohasimiana nchini Sudan zinatarajiwa kuanza kutekeleza mkataba wa usitishaji mapigano waliotiliana saini mjini Jeddah, Saudi Arabia mwishoni mwa juma lililopita, kumeripotiwa mapigano katika baadhi ya maeneo, hali inayoibua maswali ikiwa mkataba huo utadumu.

Kifaru cha kivita cha jeshi la Sydan kusini mwa mji wa Khartoum  Mei 21, 2023 (Photo by AFP)
Kifaru cha kivita cha jeshi la Sydan kusini mwa mji wa Khartoum Mei 21, 2023 (Photo by AFP) AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya kusitisha mapigano, yametiwa saini na wawakilishi wa jeshi na wale wa wapiganaji wa RSF, baada ya mazungumzo ya mjini Jeddah na sasa yataanza kutekelezwa rasmi kuanzia siku ya Jumatatu.

Chini ya makubaliano haya, mbali na usitishwaji wa mapigano, pande hizo mbili zitatakiwa kutuhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa raia walionaswa kwenye mapigano.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema, haifahamiki ikiwa mkuu wa majeshi ya Sudan jenerali Abdel Fattah al Burhani na mwenzake anayeoongoza kundi la RSF Mohamed Dagalo, watakuwa tayari kuheshimu makubaliano ya safari hii.

Maelfu ya raia wa Sudan wametorokea katika nchi jirani kama vile Chad na Sudan Kusini wakihofiwa mapigano yanayoendelea (Peter Louis/WFP via AP)
Maelfu ya raia wa Sudan wametorokea katika nchi jirani kama vile Chad na Sudan Kusini wakihofiwa mapigano yanayoendelea (Peter Louis/WFP via AP) AP - Peter Louis

Haya yanajiri wakati huu umoja wa Mataifa ukisema hadi kufikia mwishoni mwa juma hili, watu zaidi ya milioni 1 na laki moja wamekimbia makazi yao na wengine kuwa wakimbizi kwenye nchi jirani.

Pande hizo hasimu za kijeshi zimekuwa zikisisitiza kuendelea na vita, kila mmoja akidai kuwa lengo lake ni kuibuka mshindi katika vita ya kuwania madaraka yanyoendelea na ambapo imeingia wiki ya 6.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.