Pata taarifa kuu

WFP yatoa wito wa msaada wa dharura kwa Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linazindua wito wa dharura kwa Mali, hasa kwa jimbo la Ménaka. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumatano, Mei 17, shirika hilo linaeleza kuwa linahitaji ufadhili wa haraka wa dola milioni 110 "ili kuongeza msaada wake wa dharura wa chakula na lishe".

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limetangaza kwamba ni lazima "kuharakisha shughuli zake" katikati, kusini-mashariki na kaskazini mwa Mali, kutokana na mlipuko wa watu waliokimbia makazi yao. Huyu ni mmoja wa wakimbizi wa ndani katika kambi ya Faladie, Mei 14, 2019.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limetangaza kwamba ni lazima "kuharakisha shughuli zake" katikati, kusini-mashariki na kaskazini mwa Mali, kutokana na mlipuko wa watu waliokimbia makazi yao. Huyu ni mmoja wa wakimbizi wa ndani katika kambi ya Faladie, Mei 14, 2019. © MICHELE CATTANI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Mali linataka "kuharakisha shughuli zake" katikati, kusini-mashariki na kaskazini mwa nchi, ambako raia milioni 3.8 wa Mali wanahitaji msaada wa dharura. Uimarishaji huu lazima ulenge "maeneo magumu kufikiwa kama vile Ménaka, ambapo idadi ya watu wanaoyahama makazi yao inaendelea kuongezeka", inaelezea WFP.

Katika eneo hili la kaskazini mashariki mwa Mali, mafanikio ya kundi la kigaidi la Islamic State huko Sahel kwa zaidi ya mwaka mmoja yamesababisha karibu watu 100,000 kuyahama makazi yao, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Leo, huko Ménaka, "njaa inafikia viwango vya hatari", shirika hili linaendelea. Hivi ndivyo viwango vya kutisha zaidi tangu 2014, tarehe ya kuundwa kwa "Mfumo Uliooanishwa" ambao unawezesha kuhesabu mahitaji yanayohusishwa na uhaba wa chakula.

WFP pia ina wasiwasi kuhusu kukaribia kwa maika (kati ya mavuno mawili) na "kuenea kwa ukosefu wa usalama katika mikoa ya kusini na magharibi mwa Mali, ambayo hapo awali ilikuwa salama". Kuongezeka kwa ukosefu wa usalama ambao, kulingana na WFP, "kuna madhaŕa hasi katika kilimo, uvuvi na uzalishaji wa wanyama”, na kufanya kuwa vigumu zaidi kwa familia kupata chakula. Bila kusahau kupanda kwa bei: bei ya mtama imeongezeka kwa 55%, mahindi kwa 43%, mchele kwa 27% ikilinganishwa na wastani wa miaka mitano, inabainisha WFP.

Kwa sababu hizi zote, shirika hili linasikitishwa kuwa limelazimika kupunguza mgao wake wa chakula kwa nusu, mwezi wa Aprili na Mei. "Bila ufadhili wa kutosha", WFP italazimika kupunguza mgao wake hata zaidi kuanzia mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.