Pata taarifa kuu

Sudan: Jiji la Khartoum likibaki mahame tangu kuzuka kwa mapigano

NAIROBI – Mwezi mmoja sasa tangu kuzuka kwa machafuko nchini Sudan, jiji la Khartoum likibaki mahame, milio ya risasi na mabomu vikisikika kula uchao, huku eneo la jimbo la Darfur likitumbukia kwenye mzozo mpya.

Maelfu ya raia wa Khartoum wametoroka wakihofiwa kushambuliwa katika mapigano yanayoendelea
Maelfu ya raia wa Khartoum wametoroka wakihofiwa kushambuliwa katika mapigano yanayoendelea AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Raia kwenye jijini la Khartoum, kwa majuma kadhaa sasa wanapitia kipindi kigumu cha maisha ikiwemo uhaba wa bidhaa za vyakula, mawasiliano kukatika mara kwa mara, umeme na mfumuko wa bei usiohimilika.

Jiji la watu karibu milioni 5, ambalo kwa muda mrefu limeshuhudia utulivu, sasa limekuwa uwanja wa mapambano, hakuna ndege inayoruka wala kutua, benki, hospitali, maduka na ofisi za balozi mbalimbali zikifungwa, huku kwa wahalifu huu umekuwa mwanya kwa wao kupora.

Katikati ya yote haya ni kuibuka kwa machafuko mapya kwenye jimbo la Darfur, ambapo mji wake mkuu wa El Geneina unashuhudia makabiliano kati ya jamii hasimu, mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa huku mifumo ya afya ikivurugika.

Makabiliano yaliyoripotiwa siku ya Jumatatu kati ya vikosi hasimu, yanazidisha maswali kuhusu ikiwa kuna nia ya dhati ya kupata suluhu ya mzozo unaoendelea kati ya kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah al Burhan na mwenzake jenerali Mohamed Daglo, anayeongoza wapiganaji wa RSF.

Haya yanajiri licha ya juhudi zinazoendelea kufanyawa na Saudi Arabia, ambayo inawakutanisha viongozi kutoka pande mbili zinazovutana, huku hata hivyo matumaini yakiwa ni kiduchu ikiwa kutakuwa na muafaka wowote wa kukomesha vita.

Mapigano yalizuka April 15 kati ya mkuu wa majeshi ya Sudan na aliyekuwa naibu wake ambaye anaongoza vikosi vya RSF, wote wawili wakiwania kuongoza taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.