Pata taarifa kuu

Sudan: Jeshi lafunga akaunti za benki za RSF na washirika wao

NAIROBI – Kiongozi wa jeshi la Sudan jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa agizo la kufungwa kwa akaunti za benki zinazomilikiwa na wapiganaji wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) na zile za makampuni yanayohusishwa na kuni hilo.

Abdel Fattah al-Burhan, Mkuu wa jeshi la Sudan
Abdel Fattah al-Burhan, Mkuu wa jeshi la Sudan © ASHRAF SHAZLY/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika agizo lake la Jumapili ya wiki jana, Kiongozi huyo pia aliaangiza kusimamishwa kazi kwa maofisa wanne wa jeshi wanaohusishwa na kundi hilo la RSF.

Mmoja wa maofisa walioathiriwa ni Brig Jenerali Omar Hamdan Ahmed, kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, na ambaye kwa sasa anaongoza ujumbe wa kundi hilo la RSF kwa mazungumzo ya amani na jeshi la Sudan mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Jeshi limefunga akaunti za benki za jenerali Mohamed Hamdan Dagalo na washirika wake
Jeshi limefunga akaunti za benki za jenerali Mohamed Hamdan Dagalo na washirika wake AFP

Vile vile Jenerali Burhan pia alimfuta kazi gavana wa benki kuu Hussain Yahia Jankol na kumteua Borai El Siddiq badala yake bila kutoa sababu ya kufuta kazi Jankol.

Haya yanajiri ikiwa ni siku tatu baada ya jeshi na wanamgambo wa RSF kutia saini mkataba wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa kawaida, mapigano yakiripotiwa kuendelea jijini Khartoum.

Mazungumzo zaidi ya kujaribu kusitisha vita vya mwezi mmoja sasa ambavyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 700, yanatarajiwa kurejelewa leo katika mji wa Jedda nchini Saudi Arabia.

Mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo wa Sudan yanatarajiwa kurejelewa tena nchini Saudi Arabia
Mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo wa Sudan yanatarajiwa kurejelewa tena nchini Saudi Arabia AP - Marwan Ali

Roland Marchal ni mtafiti kutoka Kituo cha Kimataifa kuhusu sayansi ya siasa jijini Paris.

“Hakika hakuna anayefuata makubaliano ya hivi karibuni, jeshi linaendelea kurusha mabomu, RSF nao wanaendelea kupigana, wote wanaendelea kupigana ndani ya mji wakiwa na nia ya kuwafanya raia kama kinga.” alisema Roland Marchal, mtafiti kutoka Kituo cha Kimataifa kuhusu sayansi ya siasa jijini Paris.

00:31

Roland Marchal kuhusu Sudan

Aidha Roland Marchal alieleza kuwa kila upande unajaribu kuuteka mji hatua aliyoitaja kuwa shida kwa jenerali Abdel Fattah al-Burhan pamoja na ndege za kivita kushindwa kushambulia.

Haya yanajiri wakati huu taarifa ya umoja wa mataifa ikieleza kuwa mapigano ya mwezi moja sasa kati ya pande mbili za kijeshi nchini humo yasababisha zaidi ya raia milioni moja kuyatoroka makazi yao.

Maelfu ya raia wameripotiwa kuyahama makazi yao nchini Sudan kutokana na mapigano kati ya jeshi la wapiganaji wa RSF
Maelfu ya raia wameripotiwa kuyahama makazi yao nchini Sudan kutokana na mapigano kati ya jeshi la wapiganaji wa RSF REUTERS - EL TAYEB SIDDIG

Mapigano kati ya pande mbili za kijeshi yameendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha kwa vita, kila upande ukituhumu mwengine kwa kuvunja mkataba wa makubaliano yenyewe.

Makabiliano kati ya jeshi la Sudan chini ya uoongozi wa Abdel Fattah al-Burhan yaliaanza tarehe 15 ya mwezi Aprili mwake huu na kundi linalomuunga mkono kiongozi wa wapiganaji wa RSF Mohamed Hamdan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.