Pata taarifa kuu

Guinea-Bissau:Kampeni kuelekea uchaguzi wa wabunge zimeanza

Nairobi – Waziri mkuu wa Guinea-Bissau, Nuno Gomes Nabiam, hapo jana alianza kampeni za uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge wa tarehe 4 Juni.

Waziri mkuu wa Guinea Bissau Nuno Gomes Nabiam
Waziri mkuu wa Guinea Bissau Nuno Gomes Nabiam REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Nuno Gomes Nabiam anafanyia kampeni chama chake, Assembly of the United People - Democratic Party of Guinea-Bissau.

Hatuwezi kuwa na maneno ya uchochezi, hiyo haisaidii, hizi hotuba zinaleta matatizo na nchi inataabika, mimi Nuno sitegemei kuleta mkanganyiko, siko hapa kwa ajili hiyo.Kuwa na uwezo wa kufanya mambo mengine. Ikiwa sipo katika siasa, nitafanya kazi nyingine. Inabidi tusimamie namna yetu ya kuwa na kufanya siasa

alisema waziri mkuu akizungumzia suala la usalama na utulivu nchini Guinea-Bissau.

Mnamo Februari 1, 2022 shambulio dhidi ya Ikulu ya Serikali, ambapo mkutano wa Baraza la Mawaziri ulikuwa unafanyika, pamoja na uwepo wa wajumbe wa mtendaji na Rais wa Guinea, Umaro Sissoco Embaló, ulisababisha vifo vya zaidi ya kumi na kuchukuliwa na mamlaka kama jaribio la mapinduzi.

Ijumaa iliyopita, vyama vya siasa vilitia saini kanuni za maadili mjini Bissau, zinazofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, ambapo zinajitolea, miongoni mwa mambo kadhaa, kukubali matokeo ya uchaguzi yaliyowasilishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Guinea-Bissau, ni nchi ambayo inaendelea kukabiliwa na mgogoro wa kisiasa kwa miaka kadhaa.

Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo, miezi miwili iliyoisha alivunja bunge la nchi hiyo na kusema kuwa utaitishwa uchaguzi wa mapema mwaka huu ili kutatua mzozo wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu.

Mvutano kati ya bunge na urais umelikumba taifa hilo la Afrika magharibi kwa miezi kadhaa. Embalo alitaja tofauti zinazoendelea na zi-sizoweza kutatuliwa na bunge, ambazo alielezea nafasi ya siasa za msituni na njama.

Rais alisema kuwa Mgogoro huo wa kisiasa umemaliza mtaji wa uaminifu kati ya taasisi huru, na sasa ameamuwa kurudisha nafasi kwa wa-Guinea ili mwaka huu waweze kuchagua kwa uhuru bunge wanalotaka kuwa nalo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.