Pata taarifa kuu

Sudan: Mazungumzo ya upatikanaji wa amani kurejelewa tena

NAIROBI – Nchini Sudan, wanajeshi na wanamgambo wa RSF wanatarajiwa kurejelea mazungumzo hapo kesho nchini Saudi Arabia, wakati huu vikosi vyote viwili vikiendelea kupambana jijini Khartoum.

Viongozi wa makundi mawili ya kijeshi yanayopigana nchini Sudan
Viongozi wa makundi mawili ya kijeshi yanayopigana nchini Sudan AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia wa Saudi Arabia amesema, kurejelewa kwa mazungumzo hayo, kunatarajiwa kusaidia kupatikana kwa upatikanaji wa maelewano ya pande zote mbili, kuacha kupigana.

Aidha, amesema kiongozi wa serikali ya Kijeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amealikwa kushiriki kwenye mkutano wa viongozi wa kiarabu, kitakachofanyika jijini Jeddah, Ijumaa ijayo, lakini ripoti zinasema hatoondoka Khartoum kwa sababu za kiusalama.

Wiki hii, pande hizo mbili zilikubaliana kuruhusu misaada ya kibinadamu kama chakula na dawa kuwafikia watu waliaothiriwa na vita vinavyoendelea, lakini hakuafikiana kuacha mapigano.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa, vita kati ya jeshi na wanamgambo hao wa RSF yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 750 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, huku zaidi ya Laki Mbili wakikimbilia nchi jirani na wengine wakikimbilia katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Watu Zaidi ya milioni moja wameripotiwa kutoroka katika mji wa Khartoum peke tangu kuaanza mapigano hayo kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa.

Raia katika mji huo wa Khartoum wanakabiliwa na changamoto za kupata matibabu baada ya hosipitali kuporwa wakati wa makabiliano kati ya wanajeshi wa wapiganaji wa RSF.

Haya yanajiri wakati huu Sudan ikitoa wito kwa jamii ya kimataifa ikiwemo umoja wa mataifa, umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda kutoa msaada wa kibindamu kwa raia wa taifa hilo .

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ameeleza matumaini yake kwamba mazungumzo yanayofanyika mjini Jeddah yataleta suluhu ilikuwasaidia walioathirika na mapigano yanayoendelea

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.